Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (469)
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Huku uvamizi na mauaji ya halaiki mjini Gaza, yakiendelea kwa muda wa miezi 23, yamefikia kilele kwa matumizi ya silaha ya njaa inayoangamiza watu pamoja na majaribio ya mbinu mpya za mauaji zinazoitwa “mabomu ya roboti”; siasa za kinyonyaji na za kinafiki za watawala wa nchi za Kiislamu—wanaokabiliwa na ghadhabu za watu wao wenyewe kwa kuitelekeza Gaza—pia zimefikia kilele cha vilele.
Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, Amerika imejidhihirisha kama mpangaji mkuu nyuma ya baadhi ya mizozo ya kunyama na ya ghasia zaidi kote duniani. Kutoka Urusi na Ukraine hadi India na Pakistan hadi China na Taiwan hadi Syria, Iraq, Afghanistan, Yemen, Kenya, Mali, Cameroon, na hii ni mifano michache tu! Hata hivyo, hakuna kilichoifichua Marekani zaidi ya uungaji mkono wake usio na haya na ushiriki wake katika mauaji ya halaiki yanayotokea Gaza dhidi ya watu wa Palestina. Kabla ya uvamizi, kuzingirwa kabisa, na kuangamizwa kwa Gaza, watu wengi hawakujua jinsi serikali ya Marekani ilivyokuwa chafu na jinsi wanavyoweza kuwatembeza wachezaji kama poni kwenye bao la chess.
Tunajua kwamba mkakati wa Marekani wa kuasisi umbile la Kiyahudi katika moyo wa nchi za Kiislamu, kwa sehemu kubwa, umeegemezwa kwenye suluhisho la dola mbili. Hata hivyo, chini ya Trump, mkakati huu umeanza kuatelekezwa, au angalau kunyamaziwa, jambo ambalo limezua maswali. Kwa mfano, Trump alisema, "Unapotazama ramani, ramani ya Mashariki ya Kati, 'Israel' ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na ardhi hizi kubwa mno. Kwa hakika nilisema: 'Je, kuna njia yoyote ya kupata zaidi? Ni ndogo..." (Sky News, 19/8/2024). Je, hii inamaanisha kuwa mradi wa suluhisho la dola mbili wa Amerika umekufa na kukamilika, au bado ungali hai?
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia itafanya mkutano na waandishi wa habari wenye kichwa: “Hizb ut Tahrir inatoa Wito kwa Serikali na Upinzani Kuzungumza kwa Sauti Moja”
Sayari ya Dunia, na hasa Bara Arabu, lilikuwa likiishi katika giza kuu lililofanya maisha ya binadamu yafanane na kuzimu. Kulikuwa na giza katika nyanja za itikadi, siasa, uchumi, mahusiano ya kijamii, na nyanja zote za maisha. Vita viliwasaga watu bila sababu, wenye nguvu walikuwepo huku wanyonge wakipotea na kutokuwepo, dhulma ilitanda maeneo yote, na utumwa ulifikia viwango vyake vya chini kabisa na vya udhalilishaji kabisa.
Mkakati na sera ya Wakoloni wa Magharibi kuelekea Umma wa Kiislamu imejikita katika kupiga vita Uislamu kama fahamu ya kihadhara na kimfumo. Ilifanya kazi kupitia njama kubwa na ovu za kuivunja Dola ya Kiislamu, kuikata vipande vipande, na kuzuia kuregea kwake madarakani na kuwaunganisha Waislamu. Ili kutekeleza sera na njama zake, Wakoloni wa Magharibi waliwaajiri baadhi ya wana wa Waislamu, wakiwalea kwa uangalifu katika fikra, siasa, utawala na vyombo vya habari. Kama vile orientalisti mmoja alivyosema, “Mti wa Uislamu lazima ukatwe kupitia mmoja wa watoto wake.”
Mashambulizi ya droni za jeshi la Pakistan katika majimbo ya Khost na Nangarhar nchini Afghanistan yamesababisha vifo vya watoto watatu kutoka kwa familia moja na kujeruhi wengine watano, wakiwemo wanawake na watoto.
Wanafunzi jumla wa Chuo Kikuu cha Dhaka, Chuo Kikuu cha Jahangirnagar, na Chuo Kikuu cha Rajshahi wametarajia kwa nguvu mabadiliko chanya ya kisiasa na uhakikisho thabiti wa ustawi wa wanafunzi baada ya uchaguzi uliodumu kwa muda mrefu wa vyama vyao vya wanafunzi mnamo Septemba. Wanafunzi wengi wa vyuo vikuu hivi walisema kwa uthabiti kwamba walitaka kukomeshwa kwa mila za unyonyaji za siasa za vyuo vikuu, na kuwataka wawakilishi wa wanafunzi wanaokuja kufanya kazi kwa ajili ya kulinda haki za wanafunzi. Walisisitiza kwamba wawakilishi wa wanafunzi waliochaguliwa lazima wawe sauti ya wanafunzi jumla ili kuhakikisha mazingira rafiki kwa wanafunzi katika vyuo vikuu kufuatia mabadiliko ya kisiasa ya Julai 2024 yaliyopatikana kupitia uasi mkubwa ulioongozwa na wanafunzi uliopindua utawala wa Awami League mnamo Agosti 5 mwaka huo.
Kwa kutolewa kwa agizo kuu na Donald Trump, jina la Wizara ya Ulinzi ya Marekani lilibadilishwa rasmi kuwa “Wizara ya Vita.” Haya hayakuwa tu mabadiliko ya jina; iliweka wazi fikra ya uvamizi ya dola za kikoloni na sera ya nje ya nchi za Magharibi inayoongozwa na ukaliaji kimabavu. Trump alisema wazi wazi: “Ulinzi ni wa kujihami sana ... lakini tunataka kuanza mashambulizi pia.”