Ukumbusho kwa Waislamu kuhusu Utakatifu wa Muislamu: Damu Yake, Mali Yake, na Heshima Yake
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vyombo vya habari vilisambaza habari za uhalifu wa kutisha uliotokea katika mji wa Al-Fashir nchini Sudan, wa mauaji, ubakaji, na uhamishaji uliosababisha maelfu ya familia kuhama. Na swali linalojitokeza ni: je, inawezaje kuwa rahisi kwa Muislamu anayeshuhudia kwamba hakuna mola wa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na anaamini Siku ya Mwisho—inawezaje kuwa rahisi kwake damu ya ndugu yake Muislamu, mali yake, na heshima yake?!



