Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Ilifanya Kisimamo na Hotuba ya Hadhara huko Nile Mashariki jijini Khartoum
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan huko Nile Mashariki jijini Khartoum walifanya, mnamo Jumamosi, 10/01/2026, kisimamo na hotuba ya hadhara ya kisiasa huko Souq Sitta. Hotuba hiyo ilitolewa na Ustadh Hammad Al-Dayi, mwanachama wa Hizb, ambapo alielezea ubora wa Ummah huu, ambao ulitimiza wajibu wake katika kuwaongoza wanadamu chini ya Dola ya Khilafah, hadi ilipovunjwa na mkoloni kafiri mnamo Rajab 1342 H. Aliukumbusha Ummah kuhusu tukio hili uchungu, na jinsi, kwa kuvunjwa Khilafah, ulivyompoteza Imam ambaye ni ngao, umoja wake na kuchanika vipande vipande, na mkoloni kafiri akapata udhibiti juu yake ili kugawanya ardhi zake.



