Jumanne, 13 Muharram 1447 | 2025/07/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Sudan imekua Jeraha jengine Chungu kwa Umma wa Kiislamu

Mnamo tarehe 18 Februari 2025, kikosi cha Rapid Support cha Sudan kilifanya mkutano katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta (KICC) jijini Nairobi kuzungumza uundaji wa serikali ya umoja ya majimbo yanayodhibitiwa na kikosi hicho nchini Sudan. Utawala nchini Kenya unashikilia kudai kwamba kujihusisha kwake kwenye mazungumzo hayo ni kuimarisha “juhudi za amani nchini Sudan”. Nairobi imetetea uamuzi wake wa kuwa mwenyeji wa kufanya mazungumzo na kikosi cha wapiganaji yanayolenga kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa. Maafisa wa Kiutawala wa Sudan wameiona hatua hii kama jaribio la kuanzisha utawala mwengine sambamba na ule wa Khartoum, hatua hii ya Kenya imepelekea kulaumiwa kwake kwa kukiuka ubwana wa Sudan na kujihusisha na matendo ya kiuhasama.

Soma zaidi...

Kuanzia Mjumuiko wa “Matembezi kwa ajili ya Khilafah” yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir, watu wanaopenda Uislamu wanawaita watoto wao wa kiume katika jeshi kujitokeza ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume; Na ili kuiridhisha Marekani na India, vib

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 tarehe 3 Machi, 2025, ya kuondolewa kwa Khilafah tukufu, Hizb ut Tahrir, Wilayah Bangladesh, iliandaa mjumuiko wa “Matembezi kwa ajili ya Khilafah” mnamo siku ya Ijumaa, Machi 7, 2025, baada ya Ijumaa, kutoka kwenye Lango la Kaskazini la Baitul, wakitaka kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume. Maelfu ya watu wanaopenda Uislamu kutoka matabaka mbalimbali walishiriki kwa hiari katika mjumuiko huu, wakipuuza vitisho vya vibaraka wa Marekani-India. Kutokana na mkusanyiko huu, watu wanaopenda Uislamu waliwaita watoto wao wanaotumikia jeshi kutoa nusrah (msaada wa kimada) kwa uongozi wa dhati wa Hizb ut Tahrir, katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

Soma zaidi...

Muandamo wa Mwezi kwa Ramadhan na Idd: Wito wa Kiwahyi wa Umoja

Kufunga ni (Ibada Tawqifiyah) “kama ilivyofaradhishwa ibada na Mwenyezi Mungu”; lengo lake lililoelezwa katika Aya “Ili mpate Taqwa” ili kujenga uchamungu binafsi na kuimarisha mafungamano ya jamii. Hadith hiyo ya Mtume Muhammad (saw) ilianzisha namna ya kufanya Ibada hii – Ibada – kwa maandiko, matendo na idhini ya (saw). Kama vile swala, zaka, na kuhiji, saumu ni Ibada ya mtu binafsi kama ilivyo ibada ya pamoja. Kufunga hutuleta pamoja kama ummah, tukiunga kama jengo thabiti. Lakini cha kusikitisha ni kwamba, tumetoka katika kusudi hili la uchamungu na umoja!

Soma zaidi...

Mkutano wa Cairo Unathibitisha Usaliti wa Watawala wa Kiarabu kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Mkutano huo wa dharura wa Waarabu ulifanyika jijini Cairo katikati ya mazingira machungu ambayo Umma wa Kiislamu unapitia, hasa hujuma za Kiyahudi mjini Gaza, na shinikizo la kimataifa linaloongezeka kuhusu kadhia ya Palestina. Kama ilivyotarajiwa, mkutano huo ulitoa taarifa ya mwisho ambayo ilikuwa na maneno ya kulaani na kukashifu, na kutaka masuluhisho ya viraka ambayo hayashughulikii mizizi ya mgogoro huo. Je, tunautazamaje mkutano huu? Na ni upi msimamo juu ya matokeo yake?

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Kongamano la kila Mwaka la Khilafah: “Kujenga Mustakabali pamoja na Khilafah kutoka Istanbul hadi Al-Qudsi!”

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 104 Hijria ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah (miaka 101 M), Hizb ut Tahrir/Wilayah Uturuki iliandaa Kongamano la kila mwaka la Khilafah kwa ushiriki mpana chini ya kichwa: “Kujenga Mustakabali pamoja na Khilafah kutoka Istanbul hadi Al-Qudsi!”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Ramadhan ya Mwaka Huu, ni Wakati wa Ukombozi (Tahrir) kutoka kwa Ukoloni wa Kijeshi!

Shirika la habari la Reuters liliripoti mnamo Februari 21, 2025 kwamba “Marekani imetoa dolari milioni 397 kusaidia mpango wa kijeshi katika chini ya Pakistan yenye silaha za nyuklia, huku msaidizi mmoja wa bunge akisisitiza kwamba matumizi ya F-16 ya Marekani katika operesheni za kukabiliana na ugaidi yatafuatiliwa isipokuwa dhidi ya India.” Huu ndio uhalisia wa ukoloni wa kijeshi: kuyafanya majeshi ya Waislamu kupigana wao kwa wao, huku wakiyazuia kupigana jihad dhidi ya India, umbile la Kizayuni, na majeshi ya Msalaba!

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu