Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 547
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mabadilishano ya makombora kati ya Pakistan na India yanaendelea katika njia nyingi za kusitisha mapigano huko Kashmir baada ya India kushambulia kwa mabomu maeneo tisa ndani ya Pakistan usiku wa Mei 6, ambayo ilisema ni "miundombinu ya kigaidi iliyohusika na shambulizi la silaha huko Kashmir" mwezi uliopita. Suluhisho la kivitendo la kusonga mbele haliwezi kuwa mzozo mdogo, lakini lazima liwe ukombozi wa kina wa maeneo yanayokaliwa kimabavu.
Mnamo Mei 5, 2025, balozi wa umbile la Kiyahudi nchini India, Reuven Azar, akitoa maoni yake juu ya shambulizi la Bahalkam, lililotokea mnamo 22 Aprili, alisema, "Tumedhamiria kusonga mbele kutetea misingi yetu, kanuni zetu na maadili yetu, na nina hakika kwamba India itafanya vivyo hivyo."
Neno “dola ya kina” (deep state) limetumika sana miongoni mwa wanasiasa na katika vyombo vya habari. Hata hivyo, katika kuchunguza kauli hizi, inadhihirika kwamba ziko tofauti. Je, unaweza kufafanua zaidi uwezekano wa maana ya suala hili ili tuweze kuelewa uhalisia wa kisiasa kuhusiana na neno hili, na kutoa baadhi ya mifano kwa ufafanuzi zaidi?
Hizb ut Tahrir/Wilayat Uturuki inaandaa kongamano la halaiki lenye kichwa “Kongamano Kubwa la Gaza” jijini Ankara, ambapo suluhisho la kweli na la kudumu la kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) litajadiliwa.
Ufalme wa Oman, ambao unaendesha upatanishi katika mazungumzo ya Marekani na Iran, ulitangaza mnamo Alhamisi (kuakhirishwa kwa raundi ya nne ya mazungumzo ambayo yalipangwa kufanyika mnamo Jumamosi katika mji mkuu wa Italia, Roma, "kwa sababu za kiufundi," bila kutaja tarehe mpya. Al-Sharq, 1/5/2025). Mazungumzo ya awali yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran yalianza mnamo tarehe 12 Aprili 2025 katika mji mkuu wa Oman, Muscat, kwa upatanishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Al-Busaidi.
Mnamo tarehe 14/4/2025, Shirika la habari la ‘Turk Press’ lilichapisha kwenye tovuti yake sababu za pingamizi ya umbile la Kiyahudi ya kuanzishwa kwa kambi ya anga ya Uturuki katika Uwanja wa Ndege wa T4 ndani ya ardhi ya Syria. Jarida la ‘Wall Street Journal’ lilichapisha kwenye tovuti yake tarehe 12/4/2025, kwamba Trump alionyesha nia yake ya kupatanisha wakati wa mkutano wake na Netanyahu wiki iliyopita. Je, hii ina maana kwamba umbile la Kiyahudi linaweza kuizuia Uturuki kuwa na uwepo wa kijeshi nchini Syria, licha ya makubaliano ya Uturuki na Syria? Je, Marekani ina dori katika suala hili ambayo inaweza kufafanua nia ya Trump kufanya upatanishi?
Kwa kaka zetu, baba zetu na wana wetu katika Jeshi la Pakistan: Ikiwa uongozi wenu utaegemea upande wa Umma na viongozi wenu kwa jihad, Umma mzima utakuungeni mkono. Ikiwa utaegemea upande wa Magharibi, uondoe na mutoke.