Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 575
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hii ilikuwa katika mahojiano na Kituo cha Al Jazeera mnamo 9/11/2025, ambayo kituo kilitangaza kikamilifu asubuhi ya 10/11/2025. Kutoka ardhi ya Waislamu huko Qatar, Rais wa Slovenia, Nataša Pirc Musar, anasema: “Israel ina haki ya kuwa na dola.” Swali linaloelekezwa kwa rais ni: Ni nani aliyelipa umbile hili haramu la Kiyahudi haki hii? Na je, kuna mtu yeyote anayesoma historia na hajui jinsi umbile hili lemavu lilivyoanzishwa katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina? Je, mauaji ya Mayahudi dhidi ya Waislamu, watu wa Palestina, yanaondoka akilini mwa msomaji yeyote adilifu wa historia? Umbile hili lemavu lilisimamishwaje juu ya mafuvu na maiti za watu wengi wa Palestina?
Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Palestina kilifichua, kulingana na ushuhuda mpya uliokusanywa na mawakili na watafiti wa kituo hicho kutoka kwa wafungwa kadhaa walioachiliwa huru kutoka Ukanda wa Gaza kutoka magereza na vituo vya uzuizi vya umbile la Kiyahudi, utaratibu na mpangilio wa mateso ya kingono, ikiwemo ubakaji, kuvua nguo, kulazimishwa kurekodi filamu, na unyanyasaji wa kingono kwa kutumia zana na mbwa, pamoja na udhalilishaji wa kisaikolojia wa makusudi unaolenga kuponda utu wa binadamu na kufuta kabisa kitambulisho cha mtu binafsi.
Vyombo vya habari ndani na nje ya Yemen vilisambaza, mnamo Jumanne, 18/11/2025, habari za kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia Masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Hamish Falconer, mjini Aden; ambapo alikutana na Rashad Al-Alimi, Mwenyekiti wa Baraza la Rais lenye wanachama wanane, na waziri huyo wa Uingereza pia alikutana na Waziri Mkuu Salem bin Buraik na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Shaya Zindani, na mawaziri kadhaa, na Mwewe huyo aliandamana na Balozi wa Uingereza mjini Aden, Abda Sharif.
Mnamo Jumatano, 5 Novemba 2025, ajali mbaya ya barabarani ilitokea katika Barabara ya Al-Arqoub katika wilaya ya Shuqra, jimbo la Abyan, kusini mwa Yemen, ambayo ilisababisha kuchomeka kwa basi la usafiri wa umma lililokuwa njiani kuelekea Aden, likitoka mji wa Jeddah, mali ya Kampuni ya Saqr Al-Hijaz, na lililokuwa limebeba abiria 42.
Baada ya kutenganishwa kwa Sudan Kusini na kaskazini mwaka wa 2011, eneo la Abyei liliachwa na utata na kutokuwa la upande wowote — Kusini au Kaskazini — hakukutatuliwa, ilhali kura ya maoni ilitakiwa kufanyika Abyei mwaka wa 2011, sambamba na kura ya maoni ya Sudan Kusini, ili kubaini uhusiano wa eneo hilo na Kaskazini au Kusini, lakini kura ya maoni haikufanyika kwa sababu ya mzozo wa dola hizo mbili kuhusu nani ana haki ya kupiga kura katika kura ya maoni! Eneo hilo linakaliwa na makabila ambayo ni ya Kusini, yaani kabila la Dinka Ngok, na mengine ambayo ni ya Kaskazini, yaani kabila la Misseriya, na bila shaka Wadinka hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kaskazini kwa sababu wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika Dola ya Sudan, na vivyo hivyo Wamisseriya hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kusini kwa sababu wao pia wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika dola hiyo.
Sudan imeshuhudia mabadiliko makubwa katika vita vyake, ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya miaka miwili, huku Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikichukua udhibiti wa El Fasher, ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan. Hii imeimarisha udhibiti wao katika eneo hilo. Mapigano sasa yamejikita katika eneo jirani la Kordofan.
SNAP (Programu ya Usaidizi wa Lishe ya Ziada) ni mpango wa shirikisho unaowasaidia watu binafsi, familia, na wale wenye ulemavu kupata manufaa ya kielektroniki ambayo hutumika kwa chakula, vinywaji visivyo na kileo, na mimea kukuza chakula chao wenyewe. Inaripotiwa kuwa kuna Wamarekani milioni 42 ambao hutegemea manufaa ya SNAP kujilisha wao wenyewe na familia zao. 54% ya watu wazima wanaopokea manufaa ya chakula ni wanawake, hasa kina mama wasio na waume, na 39% ni watoto, ambayo ina maana kwamba takriban mtoto 1 kati ya 5 hutegemea manufaa haya ili kuhakikisha hawalali njaa.