Jumatatu, 16 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  12 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 24
M.  Alhamisi, 04 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maslahi ya Nani Yanatumikiwa kwa Uamuzi wa Serikali wa Kufungua Tena Kivuko cha Mpakani cha Adre huku Watu wa Fashir Wakifa kwa Njaa?!

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Sudan ilitangaza mnamo Jumanne kwamba itaongeza muda wa ufunguzi wa kivuko cha mpakani na Chad cha Adre kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu hadi mwisho wa mwaka huu. Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa taarifa ikisema kwamba hatua hii inathibitisha dhamira ya serikali ya kuhakikisha kwamba misaada ya kibinadamu inawafikia wale wanaohitaji nchini kote, na kuonyesha nia yake njema katika kuwezesha shughuli za kibinadamu.

Kivuko cha mpaka cha Adre kinachukuliwa kuwa mojawapo ya vivuko muhimu zaidi kati ya Sudan na Chad. Ingawa serikali ilikuwa imetuhumu Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwa kutumia kivuko hicho kama njia ya usambazaji wa vifaa vya kijeshi na kwa kusafirisha silaha kwa kisingizio cha misaada ya kibinadamu, iliendelea kupanua idhini kwa kivuko hicho kubaki wazi kila baada ya miezi mitatu, kuanzia Agosti 2023 na kuhitimishwa na upanuzi huu wa hivi karibuni. Hili lilifanyika chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa Marekani, ambayo ilitaka kuwekwa wazi kivuko hicho ili kuhakikisha njia endelevu ya usambazaji kwa RSF. Serikali pia ilikuwa imetuhumu nchi zisizotajwa majina na mashirika ya kimataifa kwa kutumia kivuko cha Adre kusafirisha vifaa vya kijeshi na mafuta hadi RSF. Harith Idris, mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, alifichua kwamba takriban magari 25 ya kijeshi na malori manane yaliyokuwa yamebeba zana za kijeshi yaliingia Sudan kupitia kivuko hicho mnamo Mei 26, 2023, chini ya pazia la misaada ya kibinadamu. Pia aliripoti kwamba malori manane yaliyokuwa yamebeba vifaa vya kijeshi kwa ajili ya RSF yaliingia katika mji wa Geneina kupitia kivuko hicho mnamo Juni 2, 2023. Haya, pamoja na ushahidi mwengine, yaliwasilishwa na mkuu wa ujumbe huo kwa Baraza la Usalama.

Ukweli huu unathibitisha kwamba Marekani, pamoja na mawakala wake ndani ya Umoja wa Mataifa na kwengineko, wanatumia pazia la misaada ya kibinadamu kuimarisha Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ili waweze kuimarisha udhibiti wao juu ya Darfur yote, kufungua njia ya kujitenga. Hii ni hali ile ile iliyotumika katika kujitenga kwa Sudan Kusini, wakati silaha zilisafirishwa kwa waasi kupitia usafirishaji unaodaiwa kuwa wa kibinadamu. Cha ajabu, hata hivyo, ni tabia ya serikali; inajua haya yote, lakini inatii shinikizo la Marekani na kufungua sehemu hii muhimu ya kuvuka! Zaidi ya hayo, misaada hii inayoitwa ya kibinadamu haiwafikii wale wanaoihitaji sana. Je, serikali inatumikia maslahi ya nani kwa kufungua kivuko cha Adre wakati watu wa Fashir wanakufa kwa njaa na kipindupindu kutokana na mzingiro unaonyonga uliowekwa na RSF kwa Fashir na kambi za IDP zinazoizunguka kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa?

Wajibu wa serikali ni kuzuia njama hii chafu ya Marekani, ambayo inalenga kutenganisha Darfur na Sudan, kama ilivyotokea hapo awali kwa Sudan Kusini. Ni lazima isinyenyekee kwa amri za wakandamizaji, dola za makafiri, hasa Marekani. Serikali lazima ifanye kazi kwa bidii ili kuondoa mzingiro wa Fashir na kukomboa kila shubiri ya eneo la Sudan kutoka kwa waasi, kwani inao uwezo wa kufanya hivyo.

Watu wetu wa Sudan wana wajibu wa kidini wa kuwahisabu watawala hawa, kuwaongoza kuelekea kwenye njia iliyo sawa, na kujitahidi kuleta mabadiliko kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itatibua njama za makafiri na kuwazuia wale wanaotaka kuhujumu umoja wa nchi yetu. Kama asemavyo Mwenyezi Mungu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb Ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu