Jumatatu, 26 Muharram 1447 | 2025/07/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Jibu la Swali: Kuamiliana na Dola zilizo za Kivita Kivitendo

Ndugu mmoja aliniuliza kuhusu kufanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza makontena katika makaazi ya Barkan. Hivi majuzi, sehemu ya kiwanda hiki iligeuzwa kwa manufaa ya jeshi la ‘Israel’, na kinatengeneza matrela ya kusafirisha majenereta ya umeme na vitu vyengine vinavyohusiana na jeshi. Je, inajuzu kufanya kazi katika sehemu hii inayotengeneza matrela kwa ajili ya jeshi?

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Biashara ya Mtandaoni (E-Commerce)

Je, biashara ya mtandaoni (e-commerce) na kampuni ya DXN ya Malaysia inaruhusiwa? Kampuni hii inategemea uuzaji wa virutubisho vya lishe, shampoo, krimu za ngozi...nk. Unapo  nununua kutoka kwake kiasi fulani, inatoa punguzo (discount). Pindi pointi zako zikifika 100 inakupa punguzo la asilimia sita. Kadiri unavyopata pointi zaidi, ndivyo inavyokupa punguzo kubwa zaidi, na pointi hizi hubadilishwa kuwa kiasi cha pesa ambacho huhamishiwa kwako ama kwa njia ya bahasha au barua ambayo hutolewa kwako kila mwezi, au kuhamishiwa kwenye salio (balance) lako la benki.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Je, Yajuzu Mtu Kumpa Zaka Dadake au Binti Yake?

Uislamu umewajibisha kushibisha mahitaji haya ya kimsingi na kuwapa wale wasioweza kuyapata. Ikiwa mtu binafsi anajipatia wenyewe, ni vizuri; ikiwa hawawezi kujiruzuku kwa sababu ya ukosefu wa pesa za kutosha au kutokuwa na uwezo wa kupata pesa za kutosha, Shariah inawajibisha wengine kuwasaidia hadi mahitaji haya ya kimsingi yatimizwe.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Mabalozi katika Uislamu

Nina swali kuhusiana na rasimu ya katiba ya Hizb. Katika ibara ya 7 kifungu cha F inasema: "Dola itatabikisha hukmu zote za Sharia na mambo yote ya Shari'ah ya Kiislamu, kama vile miamala, kanuni za adhabu, ushahidi, mifumo ya utawala na uchumi miongoni mwa mengine kwa usawa juu ya Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, Dola pia itatabikisha hayo hayo juu ya wale walio na mkataba, wanaomba hifadhi na wale wote walio chini ya mamlaka ya Uislamu kwa njia hiyo hiyo.

Soma zaidi...

Zaka juu ya Bidhaa za Biashara

Namaanisha, zaka ya bidhaa za biashara ni thamani ya bidhaa inayotolewa kwa ajili ya kuuzwa, thamani ya kuiuza kutoka kwa mlipaji zaka kwa wateja wake, sio thamani ambayo mlipaji zaka anainunulia kwayo!

Ikiwa nilinunua simu za rununu 10,000 na kuziuza kwa 15,000. Zaka itakuwa kutokana na 15,000.

Je, hii ni sahihi?!

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu