Jumanne, 17 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uchaguzi wa DUCSU: Siasa za Kidemokrasia Zimeshindwa Kutumia Nguvu ya Vijana kwa Mabadiliko ya Kweli

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wanafunzi jumla wa Chuo Kikuu cha Dhaka, Chuo Kikuu cha Jahangirnagar, na Chuo Kikuu cha Rajshahi wametarajia kwa nguvu mabadiliko chanya ya kisiasa na uhakikisho thabiti wa ustawi wa wanafunzi baada ya uchaguzi uliodumu kwa muda mrefu wa vyama vyao vya wanafunzi mnamo Septemba. Wanafunzi wengi wa vyuo vikuu hivi walisema kwa uthabiti kwamba walitaka kukomeshwa kwa mila za unyonyaji za siasa za vyuo vikuu, na kuwataka wawakilishi wa wanafunzi wanaokuja kufanya kazi kwa ajili ya kulinda haki za wanafunzi. Walisisitiza kwamba wawakilishi wa wanafunzi waliochaguliwa lazima wawe sauti ya wanafunzi jumla ili kuhakikisha mazingira rafiki kwa wanafunzi katika vyuo vikuu kufuatia mabadiliko ya kisiasa ya Julai 2024 yaliyopatikana kupitia uasi mkubwa ulioongozwa na wanafunzi uliopindua utawala wa Awami League mnamo Agosti 5 mwaka huo. (New Age, 23 Agosti 2025).

Maoni:

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dhaka wamekuwa wakiongoza mavuguvugu mbalimbali nchini Bangladesh, kuanzia vuguvugu la lugha mwaka 1952 hadi uasi wa hivi karibuni wa Julai dhidi ya utawala dhalimu wa Hasina. Chuo Kikuu cha Dhaka kina urithi wa kihistoria wa kuunda mienendo ya kisiasa nchini Bangladesh. Kwa kawaida, matokeo ya shirika linalolinda Muungano wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dhaka (DUCSU) yanachukuliwa kuwa muhimu kisiasa katika ngazi ya kitaifa. Kwa hivyo, ni kawaida kwamba uchaguzi wa DUCSU siku zote huwa zaidi ya uchaguzi wa chama cha wanafunzi. Kwa kuwa kundi kuu la wanafunzi la chuo kikuu cha umma chenye hadhi ya juu zaidi, DUCSU daima imekuwa kitovu cha harakati zozote muhimu za kisiasa nchini Bangladesh. Uchaguzi wake unachukuliwa kuwa uwanja wa mafunzo kwa viongozi wa mustakabali. Kama vile Chuo Kikuu cha Dhaka, wanafunzi wa vyuo vikuu vyengine vya umma pia wamekuwa mstari wa mbele wa kila mabadiliko makubwa katika siasa za Bangladesh.

Wakati huu, wakati wa vuguvugu la Julai '24, tulishuhudia vijana waliojishughulisha na wanaozingatia siasa kutoka vyuo vikuu vya kibinafsi na vilevile walifanya kama kichocheo kikubwa cha mabadiliko ya serikali. Lakini tukiwa na matumaini kuhusu uwezo wa wanafunzi nchini Bangladesh, lazima pia tuelewe kwamba hakuna harakati za wanafunzi za zamani ambazo hazijaweza kutuletea mabadiliko ‘halisi’. Vyama vya kisiasa vya mfumo mbovu wa kidemokrasia vimekuwa vikitumia kujitolea kwa wanafunzi kila wakati. Kinadharia, mfumo wa kidemokrasia unapaswa kuakisi matakwa ya wananchi kwa jumla. Kwa uhalisia, mfumo wa kidemokrasia ulifeli vibaya sana kwa sababu unaasisi Ubepari unaotumikia kipote cha wanasiasa, Mabepari wachache na Wakoloni wa Magharibi. Hata tukichukulia vuguvugu la kumpinga Hasina kuwa mojawapo ya harakati zenye mafanikio zaidi katika siasa za wanafunzi wa Bangladesh, basi tunaona kwamba hamu ya vijana ya kutaka mabadiliko na kujitolea kwao tayari kumepotea mikononi mwa wabeba demokrasia hii fisidifu. Hata baada ya kuondolewa madarakani Hasina, mfumo msingi, ubepari wa kisekula, bado upo. Kipote cha watawala kinachoungwa mkono na Magharibi na mabepari wachache walafi bado kinadumisha mamlaka. Wanafunzi hasa katika Chuo Kikuu cha Dhaka, haijalishi wana shauku kiasi gani, wanalazimika kufanya kazi nje ya mfumo huu wa mamlaka. Mfumo huu fisadi wa mamlaka unafanya kazi kwa kutumia sarafu ya mabeberu mamboleo, hasa Marekani. Na, kwa bahati mbaya, mfumo wa kisiasa uliopo wa Bangladesh hauruhusu vijana wetu kufikiria na kufanya uanaharakati nje ya mfumo wa kidemokrasia.

Kwa hiyo, vijana wetu wanahitaji siasa za mabadiliko ya dhana ili kuleta mabadiliko ya kweli. Wanahitaji kuibadilisha demokrasia fisadi iliyofichwa nyuma ya pazia la 'mawazo huru', 'uhuru', 'ubinadamu' na kuweka mfumo mtukufu (wa kiungu) uliotolewa na Mwenyezi Mungu (swt) – Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Isipokuwa na hadi tuelekeze nguvu hii kubwa ya vijana wetu kupitia ushirikiano wa kisiasa wenye kujenga kwa ajili ya dola ya Khilafah, hatuwezi kuwapa watu wa Bangladesh kesho iliyo angavu na yenye mafanikio.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Irtiza Chowdhury – Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu