Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
H. 15 Rabi' I 1447 | Na: Afg. 1447 H / 04 |
M. Jumapili, 07 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutoka “Wizara ya Ulinzi” hadi “Wizara ya Vita”: Ni Wakati wa Kuchunguza upya Maana ya Ulinzi wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Kwa kutolewa kwa agizo kuu na Donald Trump, jina la Wizara ya Ulinzi ya Marekani lilibadilishwa rasmi kuwa “Wizara ya Vita.” Haya hayakuwa tu mabadiliko ya jina; iliweka wazi fikra ya uvamizi ya dola za kikoloni na sera ya nje ya nchi za Magharibi inayoongozwa na ukaliaji kimabavu. Trump alisema wazi wazi: “Ulinzi ni wa kujihami sana ... lakini tunataka kuanza mashambulizi pia.”
Nchi za Magharibi—ambazo kwa karne nyingi zilizungumza kwa lugha ya amani, diplomasia, jumuiya ya kimataifa, na ushirikiano—sasa bila aibu zinazungumza kwa lugha ya vita vya kushambulia, kama walivyokuwa wakifanya katika nyakati zao za kibeberu. Wakati huo huo, Umma wa Kiislamu, unaofungiwa ndani ya mfumo uliooza na wenye vikwazo wa dola ya kitaifa, bado umefungwa pingu na istilahi za kujihami na sera zenye mwelekeo wa kujisalimisha. Wakati fulani, Waislamu walijivunia jihad, ufunguzi, na kubeba ujumbe wa Uislamu; leo, matarajio ya juu zaidi katika ardhi ya Waislamu yamedunishwa hadi kwenye vita vya kujihami na “ukombozi kutokana na uvamizi.”
Huku Magharibi ikitangaza kwa uwazi msimamo wa uvamizi, Umma wa Kiislamu lazima uregee kwenye misingi yake. Tangu awali, dola ya Mtume (saw) mjini al-Madinah ilikuwa na msimamo—sio wa ukoloni, uhalifu, au mauaji ya halaiki kama Magharibi, bali kubeba Uislamu na kuwaongoza wanadamu. Sera ya kigeni ya Uislamu, tangu mwanzo, ilijengwa juu ya kuifanya dini idhihiri na kuvunja mipaka ya batili, ili kuwatoa wanadamu kutoka kwenye ukandamizaji wa dini (nyenginezo) hadi kwenye uadilifu wa Uislamu.
[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Al-Saff 61:9]
Kwa kweli, dhamira ya kuifanya Dini idhihiri haifungwi na mipaka wala haifahamiki ndani ya mfumo wa kisekula wa kimataifa. Uislamu uliteremshwa kwa ajili ya mamlaka ya kilimwengu. Ni wajibu wa Ummah kudhihirisha Dini kwa njia ya da’wah na jihad, ili dini ya Mwenyezi Mungu (swt) itawale dini na mifumo mengineyo. Hata hivyo kuanzia karne ya kumi na tisa na kuendelea—na hasa baada ya kuanguka kwa Khilafah—kupitia kuenea kwa utaratibu wa dola za kitaifa na kupitishwa kwa sera za ulinzi, ari ya mpango wa kuanzisha mashambulizi iliondolewa kutoka kwa Umma wa Kiislamu. Wakoloni, wakati huo huo, waliendelea na mashambulizi yao chini ya kauli mbiu za amani na utulivu: walizikalia kimabavu ardhi na, kama tunavyoshuhudia leo mjini Gaza, wameua kwa umati jamii ya Waislamu mbele ya macho ya ulimwengu. Hata hivyo, watawala wa Waislamu—ambao mawaziri wao wa vita huitwa “mawaziri wa ulinzi”—hujifunga wenyewe katika kulinda mipaka ya nchi na kuheshimu mikataba yenye vikwazo. Wakifungwa na sera za ulinzi, za kitaifa, watawala hawa wamechagua kimya, na – kuegemea fahamu za kisiasa za Magharibi – wameufanya uzembe kama huo na kurudi nyuma kuwa ni busara, ustadi, na sifa ya utawala.
Magharibi sasa inatafuta kwa mara nyengine tena kuendeleza malengo yake ya kikoloni chini ya bendera ya vita vya kuanza mashambulizi. Je, Umma wa Kiislamu—na watawala wa Afghanistan—wamejitayarisha kuweka kando majina ya kujihami na kufafanua upya dori yao? Je, wakati haujafika wa kuvunja mipaka, kujitahidi kwa ajili ya usaidizi wa waliodhulumiwa, na kuregesha jihad—sio tu kama ulinzi dhidi ya uvamizi, bali katika umbo lake pana zaidi kama njia ya sera ya kigeni—kwenye ajenda?
Hivyo basi, ni lazima tuachane na sera za kiulinzi zenye kuzingatia uchumi, “zenye mizani sawa,” na kufufua njia sahihi kwa kusimamisha Khilafah Rashida. Kwani Khilafah kwa Njia ya Utume pekee ndiyo inayoegemeza sera yake ya kigeni katika da’wah na jihad—ili Uislamu upate kutawala duniani na fitnah iondolewe.
[وَقاتِلُوهُمْ حَتّى لا تَكونَ فِتْنَةٌ وَيَكونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ] “Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu.” [Al-Baqarah 2:193]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Afghanistan |
Address & Website Tel: http://hizb-afghanistan.org/ |
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org |