Vikosi vya Pakistan Lazima Vitumwe Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Sio Kutimiza Ndoto za Adui wa Mwenyezi Mungu (swt), Trump, na Mayahudi!
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kutumwa kwa vikosi vya jeshi la Pakistani Gaza kuwanusuru watu wake na kupigana na Mayahudi ambao wameendelea na operesheni ya mauaji ya halaiki huko, tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hakukujadiliwa kamwe, kwa kisingizio kwamba Gaza iko mbali, na kwamba wajibu wa Sharia wa kuinusuru unawaangukia wale walio karibu zaidi. Lakini mara tu bwana wa serikali ya Pakistan na adui wa Mwenyezi Mungu (swt), Trump, alipoamuru serikali hii kutuma vikosi ili kufikia ndoto zake mjini Gaza, ghafla Pakistan ikawa nchi jirani na Gaza, na vikosi vya jeshi la Pakistan vimewekwa tayari kufanya operesheni za kijeshi nje ya mipaka ya kitaifa ya Pakistan. Hivyo uongo wa serikali hii ulifichuliwa kuhusu kutoweza kwake kutuma vikosi vya jeshi kuwanusuru watu wetu mjini Gaza.



