- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Pakistan kwa Mara Nyengine Tena Inatekeleza Mradi wa Marekani dhidi ya Afghanistan
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mashambulizi ya droni za jeshi la Pakistan katika majimbo ya Khost na Nangarhar nchini Afghanistan yamesababisha vifo vya watoto watatu kutoka kwa familia moja na kujeruhi wengine watano, wakiwemo wanawake na watoto.
Maoni:
Matukio ya hivi majuzi katika eneo hilo yanaonyesha kuwa Pakistan imechukua tena mradi mpya unaoelekezwa na Marekani kuhusu Afghanistan. Mradi huu, mwendelezo wa sera ya muda mrefu ya Washington ya kukandamiza harakati yoyote huru ya Kiislamu katika eneo hili, sasa unafuatiliwa kwa nguvu na uratibu zaidi. Hatua za hivi karibuni za kijeshi, kidiplomasia na kijasusi za Pakistan zinaweka wazi kuwa Islamabad imechukua dori ya chombo cha shinikizo dhidi ya Afghanistan.
Ziara za hivi punde zaidi za Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Asim Munir, nchini Marekani, pamoja na mikutano ya ngazi ya juu kati ya maafisa wa Marekani na Pakistan jijini Islamabad—sanjari na ombi la Washington la kuregesha zana zilizosalia za kijeshi kutoka Afghanistan—ni sehemu ya mradi huu. Muda mfupi baada ya mikutano hii, jeshi la Pakistan lilianzisha mashambulizi ya anga kwenye maeneo ya mpaka wa Afghanistan, kuonyesha jinsi makubaliano ya nyuma ya pazia yanavyogeuzwa kuwa operesheni haraka. Mashambulizi dhidi ya maeneo ya Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP) karibu na mpaka wa Afghanistan yanaimarisha zaidi uwezekano wa ushirikiano wa kijasusi wa Marekani.
Wakati huo huo, Marekani inaweza kuwa inaunda motisha mpya ya kifedha kwa Pakistan kwa kuwezesha kwa kiasi Hazina ya Usaidizi wa Muungano (CSF) kwa ajili ya shughuli za kukabiliana na ugaidi. Wakati huo huo, maafisa wa Pakistan, akiwemo mkuu wa jeshi, wamekuwa wakisisitiza dori ya Pakistan katika “kupambana na ugaidi,” wakitaka kutoa taswira nzuri ya ushirikiano huu mpya kwa Washington.
Lengo la msingi la mradi huu ni wazi: kushinikiza Taliban, kudhibiti harakati za Kiislamu katika kanda, kusukuma mwelekeo wa kijeshi wa Pakistan kuelekea magharibi ili kuihakikishia India, na kuzuia kuibuka kwa mabadiliko yoyote ya kimsingi ambayo yanaweza kupinga mfumo wa kimataifa unaotawaliwa na Magharibi. Kwa mara nyengine tena, chini ya bendera ya kupata “maslahi ya kitaifa,” Pakistan imejiweka sawa na mradi ambao utachochea tu kukosekana kwa utulivu, kurefusha vita vya wakala, na kudhoofisha Umma wa Kiislamu.
Ikiwa hali hii itaendelea, harakati za Kiislamu katika eneo zitakabiliwa na vitisho sio kutoka kwa adui wa kigeni, lakini kutoka kwa jirani mamluki. Njia pekee ya kukabiliana na uhalisia huu ni kupitia mabadiliko ya kisiasa na kijiografia katika kanda hii kwa kusimamisha Khilafah Rashida – badala ya kung'ang'ania kile kinachoitwa “sera za kitaifa” za Pakistan.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yosuf Arsalan
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan