Ukamatwaji wa Wanachama wa Hizb ut Tahrir jijini Beirut!
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika marudio ya mbinu na hatua za ukamataji holela wa vyombo vya usalama bila msingi wowote wa kisheria, wa watu—baadaye waliotambuliwa kuwa wanachama wa chombo cha usalama chenye mfungamano na serikali—wakiwa kwenye pikipiki waliwakamata wanachama wawili wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon walipokuwa wakigawanya taarifa moja ya kulaani kuendelea kwa uvamizi wa Kiyahudi dhidi ya Lebanon na watu wake. Kukamatwa huku kulitokea jana, 17/10/2025, baada ya Swala ya Ijumaa mbele ya Msikiti wa Imam Ali katika eneo la Tariq al-Jadida jijini Beirut.



