Trump Awaongoza Wafuasi wake kutoka kwa Watawala katika Ardhi za Waislamu kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!
- Imepeperushwa katika Hizb ut-Tahrir
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
“Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha alfajiri ya Jumanne mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ukanda wa Gaza baada ya kuidhinisha rasimu ya azimio lililowasilishwa na Marekani na kuunga mkono mpango wa amani wa Trump katika sekta hiyo, na Rais Trump aliisifu kura ya Baraza la Usalama kuhusu azimio la Gaza kama wakati wa kihistoria...” (BBC, 18/11/2025). Kuhusu Azimio Nambari 2803, lilichapishwa na vyombo vya habari na lilikuwa ni idhini ya mpango wa pointi 20 wa Rais Donald Trump wa kukomesha mzozo mjini Gaza, lililotolewa mnamo tarehe 29 Septemba 2025.



