Kimbunga cha Al-Aqsa kiko Hai na Kinaendelea
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa haikuwa tukio la muda mfupi ambalo lilimalizika kwa makubaliano ya mhalifu Trump na dola ya kikafiri nyuma yake, Marekani, muungaji mkono rasmi wa umbile la Kiyahudi. Badala yake, Kimbunga cha Al-Aqsa kilikuwa ni cheche iliyowasha moto ndani ya nyoyo za Waislamu, na kuzifungua akili na nyoyo zao. Waliona unyonge na uovu wa watawala wao wasaliti, na wakatambua unafiki wa wale wanaodai kuwa ni na ubinadamu, na wanaotetea haki za wanawake na watoto. Wakawa na hakika kwamba sheria za kimataifa, na mikataba si chochote ila ni silaha inayotumiwa na makafiri, dhidi ya Uislamu na Waislamu.