Enyi Waislamu: Waokoeni watu wa Gaza Kabla Hawajaangamizwa Kabisa na Jihadharini Isije Akakushukieni Ghadhabu na Adhabu ya Mwenyezi Mungu
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Umbile la Kiyahudi linaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza, likilenga maeneo mbalimbali ya Ukanda huo kwa mashambulizi ya anga na mizinga mikubwa, na kusababisha makumi ya vifo na majeruhi kila siku. Kwa wiki kadhaa, limezidisha mashambulizi yake katika mji wa Gaza, eneo lenye wakaazi wengi na watu waliokimbia makaazi yao kutoka sehemu ya kaskazini ya Ukanda huo, kwa ajili ya maandalizi ya kukaliwa tena kimabavu. Linalenga shule na makaazi, linatekeleza operesheni kubwa za ubomoaji inayolenga nyumba zote za makaazi, na kuvunja magorofa ya makaazi, likiambatanisha na maonyo kuhamia sehemu ya kusini ya Ukanda huo.