Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Mirza Ahmadov Miraziz
- Imepeperushwa katika Uzbekistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa huzuni na majonzi makubwa, tunaomboleza kuondokewa na mwana wetu mwengine madhubuti na mchamungu, na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ndugu yetu Mirza Ahmad Mir Aziz alifariki dunia siku ya Ijumaa, 10 Oktoba 2025, na swala ya janaza iliswaliwa kwa ajili yake jana, Jumamosi. Mir Aziz alizaliwa Tashkent mwaka wa 1970. Alikuwa mmoja wa maelfu ya Waislamu wenye ikhlasi na ujasiri ambao waliitikia wito wa Hizb ut Tahrir kwa watu wa Uzbekistan kufanya kazi ya kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu.