Mwisho wa Enzi ya Awami League, Chama Kinara cha Siasa za Kisekula - ni Onyo la Kihistoria kwa Vyama Vilivyopo vya Kisiasa na Nyuso Mpya za Kisiasa
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa kuanguka kwa dhalimu Hasina na tangazo rasmi la kupigwa marufuku kwa shughuli zote za chama kiovu cha Awami League, enzi ya giza ya siasa za chama kikuu cha kisekula -Awami League imekamilika. Kuangamia huku kwa Awami League, mrithi wa 'All India Muslim League' iliyoanzishwa mwaka wa 1906, hakutokani na mlingano wa kisiasa wa mamlaka ya kundi lolote la kisiasa, bali ni ukweli wa kihistoria na usioepukika. Hamu ya Waislamu wa India ni kuishi chini ya utawala wa Kiislamu-Khilafah.