Fahali Wanapopigana, Zinazoumia ni Nyasi “Sudan ni Mfano”
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Sijapata katika historia msemo wenye ufasaha zaidi wa uovu wa ukoloni kuliko maneno ya Rabi ibn Amir, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwa kamanda wa Kifursi: “Sisi ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewatuma kuwatoa wanadamu kutoka katika ibada ya waja wengine hadi kwenye kumwabudu Mola wa waja wote.” Ijapokuwa kauli hii ilitolewa ili kubainisha lengo la ujumbe mtukufu wa Uislamu, unaowakirimu watu kutokana na kumwabudu kwao Mwenyezi Mungu, na kuhifadhi maisha yao, mali zao na heshima zao, hii wakati fulani hujidhihirisha kama kauli iliyo kinyume chake. Rehema ya Uislamu na uhuru unaowadhaminia watu unakinzana na utumwa wa watu na mataifa kwenye ukoloni, ambao unawaona kuwa ni mashini tu za kuzalisha dhahabu na pesa.