Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chazindua Kampeni ya Kimataifa “Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mgogoro wa kikatili nchini Sudan kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) wanaoongozwa na mtawala mkuu wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), ambaye hapo awali alikuwa naibu wa al-Burhan katika Baraza Kuu, sasa umeingia mwaka wake wa tatu, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia. Baadhi ya makadirio yanaweka idadi ya waliofariki katika vita hivi vya kipumbavu kufikia 150,000, huku kukiwa na ukatili wa kutisha uliofanywa na pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kinyama, mateso, ubakaji mkubwa na uhalifu mwingine wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana. Mauaji ya kikabila pia yameripotiwa, huku jamii nzima zikiteketezwa kwa moto na kuangamizwa, na mauaji ya halaiki katika miji mbalimbali, vijiji na kambi za watu waliokimbia makaazi yao.