- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Usaliti wa Magharibi kwa Wale Wanaoitumikia Katika Vita Dhidi ya Uislamu
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Al-Rayah – Toleo 563 - 03/09/2025 M
Na Ustadh Abdullah Hussein*
Mkakati na sera ya Wakoloni wa Magharibi kuelekea Umma wa Kiislamu imejikita katika kupiga vita Uislamu kama fahamu ya kihadhara na kimfumo. Ilifanya kazi kupitia njama kubwa na ovu za kuivunja Dola ya Kiislamu, kuikata vipande vipande, na kuzuia kuregea kwake madarakani na kuwaunganisha Waislamu. Ili kutekeleza sera na njama zake, Wakoloni wa Magharibi waliwaajiri baadhi ya wana wa Waislamu, wakiwalea kwa uangalifu katika fikra, siasa, utawala na vyombo vya habari. Kama vile orientalisti mmoja alivyosema, “Mti wa Uislamu lazima ukatwe kupitia mmoja wa watoto wake.”
Uingereza ilimuunga mkono Sharif Hussein katika kuanzisha Uasi wa Waarabu na kumtongoza kwa ahadi ya kuwa Khalifa. Hili lilipelekea kudhoofika, kugawanyika, na kuvunjwa kwa Khilafah Uthmani. Lengo la Uingereza lilipofikiwa, ilimgeuka, ikamnyima ahadi yake, ikamfukuza, na kumweka chini ya kifungo cha nyumbani hadi akafa kwa huzuni, kama ambavyo viongozi wote, vyama, na makundi ambao iliwatumia kuendeleza mpango wake wa kugawanya, utaifa, na kuanzisha dola bandia vibaraka.
Leo hii, Magharibi inaendelea kutumia baadhi ya Waislamu, vibaraka katika fikra, siasa, thaqafa na Dini ili kuzuia Ummah usiinuke na kuanza upya mfumo wake wa maisha wa Kiislamu. Wanatumika kukuza itikadi ya Magharibi ya kutenganisha Dini na maisha na serikali, kutoa wito wa kubadilisha Uislamu, na kueneza kile kinachoitwa “Uislamu wa Kimarekani” au “Uislamu wa Kifaransa” au “Uislamu wa Ulaya.” Wanajaribu kutilia shaka misingi ya Uislamu na kuleta mkanganyiko kuihusu. Wale wanaoitwa wanamamboleo wanashuhudia hili kwa kutoa wito wa kusoma maandiko ya wahyi kupitia fikra ya kisekula.
Kisa cha mkana Mungu wa Morocco, Rayan Bidan, ambaye alikiri wazi kwamba nchi za Magharibi zilimtumia katika vita vyake dhidi ya Uislamu, kabla ya kumtelekeza na kumtupilia mbali, inafichua ukweli mbaya wa jinsi Magharibi inavyoamiliana na wale wanaoitumikia. Pindi wanapokuwa hawafai tena, huwatupa au kuwamaliza.
Katika vita hivi dhidi ya Uislamu, nchi za Magharibi pia zinawatumia watawala wa Waislamu kutekeleza ajenda zake. Hata hivyo, licha ya utiifu wao, Magharibi kamwe haitosheki na daima hutaka zaidi!
Kwa mfano, katika kesi ya Pakistan, Waziri Mkuu wa wakati huo, Imran Khan, aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter mnamo 19/11/2018, akitetea huduma za Pakistan kwa Amerika baada ya Trump kudai kwamba Amerika ilitoa mengi kwa Pakistan lakini ilipata malipo kidogo katika vita dhidi ya “itikadi kali na ugaidi.” Imran Khan alisema, “Rekodi inahitaji kuwekwa sawa kuhusu hasira za Bw Trump dhidi ya Pakistan: 1. Hakuna Mpakistani aliyehusika katika 9/11 lakini Pakistan aliamua kushiriki katika Vita dhidi ya Ugaidi vya Marekani. 2. Pakistan ilipoteza maisha ya watu 75,000 katika vita hivi na zaidi ya $123 bilioni zilipotea katika uchumi. “Misaada” ya Marekani ilikuwa kidogo $20 bilioni.” Hivi majuzi, mnamo tarehe 24 Aprili 2025, katika mahojiano na mtangazaji wa Sky News Yalda Hakim, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, Khawaja Asif, alilalamika, “Tumekuwa tukifanya kazi hii chafu kwa Marekani kwa takriban miongo mitatu na kwa nchi za Magharibi, ikiwemo Uingereza. Hilo lilikuwa kosa na tuliteseka kwa hilo. Ikiwa tulijiunga na vita dhidi ya Muungano wa Kisovieti na baadaye, kufuatia mashambulizi ya 9/11, Pakistan ilikuwa na rekodi isiyo na dosari.” Pia alisema, “Tulipokuwa tukipigana vita tukiwa upande wao katika miaka ya 80 dhidi ya Muungano wa Kisovieti, magaidi hawa wote wa leo, walikuwa wakinywa na kula jijini Washington. Kisha ikaja 9/11. Kwa mara nyengine tena hali ile ile iliundwa. Nadhani serikali yetu ilifanya makosa.”
Hakika haya ndiyo wahyi umetujulisha, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt.):
[وَلَنْ تَرْضَى عَنْكَ الْيَهُودُ وَلا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلا نَصِيرٍ]
“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Baqarah 120]. Ukweli huu wa Qur’an unaeleza uhalisia wa Magharibi. Haijalishi ni huduma gani unayoitoa dhidi ya Dini na Ummah wako mwenyewe, siku dori yako itakapomalizika itakutupa kwenye jaa la taka au kukuangamiza. Haya si chochote ila ni hasara hapa duniani na kesho Akhera.
Kwa hiyo, Enyi wana wa Umma wa Kiislamu ambao mmejiweka katika utumishi wa duara fisadi za Kimagharibi, mkitekeleza miradi yao yenye sumu na maangamivu: Amkeni! Rudini kwenye Ummah wenu na muridhie Uislamu wenu. Fanyeni ikhlasi kwa ajili ya Uislamu, na kuweni wasaidizi kwa ndugu zenu waaminifu wanaojitahidi kuleta mabadiliko kwa kuregesha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu na kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya kipenzi Mtume (saw), kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume.
Itapindua meza ya nchi za Magharibi, itaondoa hadhara yake fisadi, itajumuisha kheri na uadilifu, na kuleta amani na utulivu.
* Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan