Amerika, Kutafuta Kuiondoa Darfur, Yaibua Suala la Abyei na Kutishia na Kuonya!
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya kutenganishwa kwa Sudan Kusini na kaskazini mwaka wa 2011, eneo la Abyei liliachwa na utata na kutokuwa la upande wowote — Kusini au Kaskazini — hakukutatuliwa, ilhali kura ya maoni ilitakiwa kufanyika Abyei mwaka wa 2011, sambamba na kura ya maoni ya Sudan Kusini, ili kubaini uhusiano wa eneo hilo na Kaskazini au Kusini, lakini kura ya maoni haikufanyika kwa sababu ya mzozo wa dola hizo mbili kuhusu nani ana haki ya kupiga kura katika kura ya maoni! Eneo hilo linakaliwa na makabila ambayo ni ya Kusini, yaani kabila la Dinka Ngok, na mengine ambayo ni ya Kaskazini, yaani kabila la Misseriya, na bila shaka Wadinka hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kaskazini kwa sababu wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika Dola ya Sudan, na vivyo hivyo Wamisseriya hawatakubali kutenganishwa na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na dola ya Kusini kwa sababu wao pia wangekuwa kiungo dhaifu zaidi katika dola hiyo.



