Alhamisi, 23 Jumada al-awwal 1447 | 2025/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mkuu wa Ujasusi wa Australia Azindua Ulinzi wa Kipumbavu kwa Umbile la Mauaji ya Halaiki

Mkurugenzi Mkuu wa ASIO, Mike Burgess, alitumia hotuba yake ya Taasisi ya Lowy jana kupanua ulinzi wa serikali ya Australia kwa umbile la mauaji ya halaiki. Burgess alitoa mkusanyiko mkubwa wa maneno yaliyopitwa na wakati, yaliyotolewa kutoka kwa serikali na wapigiaji debe wa mauaji ya halaiki, akionya kuhusu vitisho kwa mshikamano wa kijamii, kuongezeka kwa chuki dhidi ya Mayahudi na uhalalishaji wa vurugu za kisiasa. Burgess hata alifikia hatua ya kuonya kuhusu uwezekano wa mauaji ya kisiasa yanayotokana na nchi za kigeni nchini humu.

Soma zaidi...

Kutoka Uingereza hadi Australia: Utambuzi wa Uongo Unafungua Njia ya Uhalalishaji Mpana zaidi wa Mahusiano

Miaka miwili baada ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na umbile la Kizayuni katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, likiungwa mkono kikamilifu na Marekani, NATO, na washirika wao makruseda, Umoja wa Mataifa na dola zenye nguvu duniani wamejibu kwa kulituza umbile hilo. Utambuzi wa “Dola ya Palestina” unakuja huku Gaza ikivuja damu, na baada ya dola 150+ tayari kutoa utambuzi sawia.

Soma zaidi...

Kutafakari juu ya Gaza, Mfano wa Ibrahim (as) na Wito wa Haraka wa Nusrah Leo

Umma unapoingia katika siku tukufu za Tashriq, katikati ya ibada za Hijja, tunakumbushwa kwamba nguzo hii adhimu ya Uislamu ni safari ya kiroho, faradhi wa kiwahyi inayoonyesha kujitolea kipekee kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Ibada za Hijja zinajumuisha mila ya Nabii mtukufu Ibrahim (as), mke wake mtukufu Hajar (as), na mwanawe Ismail (as), familia ambayo mitihani yao iliufundisha Ummah asili ya tawakkul, imani isiyoyumba kwa Mwenyezi Mungu (swt), na kujisalimisha kikamilifu kwa amri Yake tukufu, hata pale amri hiyo inapopingana na mantiki ya kidunia.

Soma zaidi...

Hawajaridhika na Uharibifu wa Gaza, Wazayuni Sasa Wanaendeleza Uhalifu Wao hadi Lebanon

Baada ya mwaka mmoja wa kampeni ya wazi ya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Palestina, iliyofanywa mchana kweupe kwa ushirikiano wa dola za kimataifa na watawala wa Waislamu wanaowazunguka, Wazayuni hivi sasa wameendeleza jinai zao hadi Lebanon kwa kulipua mabomu kiholela katika makaazi yenye wakaazi wengi, na kuua maelfu ya watu tayari, kwa matumaini wanaweza kurekebisha sura yao iliyoshindwa baada ya kampeni yake angamivu mjini Gaza.

Soma zaidi...

Kama Umma Mmoja: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuangamizwa kwa Dhalimu Hasina na Tunawaombea Kuporomoka Madhalimu Wote Wanaoukandamiza Ummah

Baada ya majuma kadhaa ya ukandamizaji wa kikatili dhidi ya watu wa Bangladesh na dhalimu Hasina, genge la serikali yake, na wachungaji wake wa kigeni, alilazimishwa kidhalilifu kuikimbia nchi. Waislamu shupavu wa Bangladesh, wakiongozwa na wanafunzi jasiri, walivumilia ukatili usio na kifani na hatimaye kulazimisha kuondolewa kwake kupitia wimbi lisilozuilika la maandamano ambayo yalimshinda dikteta huyo.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu