Al-Waqiyah TV: Khilafah Pekee Ndio Itakayoiletea Sudan Izza!
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Sudan kwa sasa iko katikati ya vita vya kipumbavu ambavyo vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia na kuzua mgogoro mkubwa zaidi duniani wa njaa na kuhama makaazi. Wananchi wa Sudan wamekumbwa na mizozo mbalimbali pamoja na umaskini mkubwa, udikteta, migawanyiko ya kikabila na kitabaka na matatizo mengine mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa miongo kadhaa chini ya uongozi, tawala na mifumo mtawalia.