Ijumaa, 08 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  1 Jumada II 1447 Na: H 1447 / 031
M.  Jumamosi, 22 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Watoto Wafungwa Katika Magereza ya Uvamizi ni Watoto au Wanaume?!

(Imetafsiriwa)

Taasisi za Palestina zinazohusika na masuala ya wafungwa, ikiwemo Klabu ya Wafungwa, zilisema kwamba zaidi ya watoto 1630 kutoka Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na al-Quds, na makumi kadhaa kutoka Ukanda wa Gaza wamekamatwa na uvamizi tangu mwanzo wa vita dhidi ya Gaza. Waliashiria kuuawa shahidi kwa mtoto mmoja ndani ya Gereza la Megiddo baada ya kukabiliwa na njaa, kunyimwa, na unyanyasaji. 350 kati yao bado wako katika magereza ya uvamizi, wakiwemo wasichana wawili, katika hali ngumu ambazo zinagongana kabisa na viwango vyote vya kimataifa vya ulinzi wa watoto. Wanakabiliwa na uhalifu wa mateso, njaa, na kupuuzwa kimatibabu, vilevile kudhulumiwa kijinsia, pamoja na kutengwa kwa pamoja na kunyimwa kutembelewa.

Katika miongo kadhaa iliyopita, umbile nyakuzi la Kiyahudi linalojichukulia sheria mkononi limefanya maangamizi wa kimwili na kisaikolojia dhidi ya wafungwa watoto kupitia seti ya sera za kiserikali zinazogongana na maadili ya kibinadamu. Watoto wamekuwa kundi lililo hatarini zaidi kwa ukiukaji wake, iwe kupitia mauaji na majeraha, kunyimwa elimu, au kukamatwa, ambalo limewalenga makumi ya maelfu yao, iwe wakati wa uvamizi, makabiliano, katika vituo vya ukaguzi na barabarani, au kutoka shuleni. Watoto mjini Gaza mara nyingi walitumika kama ngao za kibinadamu wakati wa operesheni zake za kijeshi.

Awamu ya mahojiano inachukuliwa kuwa hatua ya kikatili zaidi kwa watoto ndani ya magereza ya uvamizi; inalenga kuwatisha, kuwavunja utashi wao, na kuwafanya kuungama. Wanahojiwa kwa masaa mingi katika vyumba vilivyofungwa bila uwepo wa wazazi wao au wakili. Wananyimwa usingizi na kupumzika, na wanakabiliwa na shinikizo endelevu ambalo linawaacha na athari kubwa kwao na mustakabali wao. Uzuiliaji wa utawala unachukuliwa kuwa mojawapo ya zana za ukandamizaji zaidi zinazotumiwa na uvamizi dhidi ya watu wa Palestina, hasa watoto, bila kufungua mashtaka wazi au kuwawasilisha katika kesi halisi, kwa kisingizio cha “faili la siri,” ambalo mtoto na wakili wake wananyimwa ufikiaji wake.

Ndani ya magereza, watoto wanaishi chini ya hali ngumu ambazo zinakosa viwango vya chini vya kibinadamu; wanakabiliwa na vipigo, shoti za umeme, kunyimwa usingizi ndani ya kile kinachojulikana kama “chumba cha disco” (muziki wa sauti kubwa), kufungwa minyororo mfululizo, mashambulizi ya mbwa, unyanyasaji wa kimaneno, kutengwa, unyanyasaji wa kijinsia, na adhabu za pamoja. Zaidi ya hayo, kuna njaa, ukosefu wa usafi, msongamano na kuenea kwa wadudu, kizuizini katika vyumba visivyo na hewa nzuri na visivyo na mwanga, pamoja na kupuuzwa kwa matibabu na ukosefu wa huduma za afya, jambo ambalo limesababisha kuenea kwa magonjwa, uhaba wa nguo, kunyimwa ziara za kifamilia, na kuwekwa kizuizini pamoja na watoto wahalifu wa Kiyahudi katika sera ya maangamizi ya kisaikolojia na kimwili.

Kwa upande mwingine, data kutoka Kampeni ya Kitaifa ya Kurejesha Miili ya Mashahidi ilionyesha ongezeko hatari la uhalifu wa kimakusudi dhidi ya watoto pamoja na sera inayoendelea ya kuzuia miili. Tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Novemba, uvamizi huo umewaua kikatili watoto sita na kuzuia miili yao, na kuongeza idadi ya watoto waliouawa ambao miili yao bado imezuiwa hadi 73 kati ya 752 ambao miili yao kampeni hiyo inarekodi kama ingali imezuiwa kwenye majokofu na makaburi ya uvamizi.

Takwimu hizi zilichapishwa na taasisi za wafungwa wakati wa sikukuu ya kile kinachoitwa “Siku ya Watoto Duniani,” ambapo ulimwengu unasherehekea mafanikio ya watoto katika nyanja zote za maisha, maendeleo yao, na ukuaji wao wa asili, huku watoto wa Palestina wakikabiliwa na mashini kandamizi inayowalenga, inakiuka haki na utu wao, inawaua, inawakamata, na kuwashtaki mbele ya mahakama za kijeshi ambapo sheria rahisi zaidi zinakiukwa, zikitoa adhabu kali mbali na kile wanachodai kuhusu haki za watoto na binadamu. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu hakika inakuja:

[لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي الْبِلَادِ * مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمِهَادُ]

“Kabisa kusikudanganye kubakia kutangatanga kwa walio kufuru katika nchi. * Hiyo ni starehe ndogo. Kisha makaazi yao yatakuwa Jahannamu. Na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia.” [Surah Aal-i Imran: 196–7].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-uttahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-uttahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu