Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 544
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Bila jeshi hata moja la Waislamu kumzuia, Trump alitimiza ahadi yake ya kufanya maangamizi makubwa Gaza. Kamera zimenasa picha za sehemu za miili ya waumini zikipaa angani, juu ya majengo marefu, kutokana na kukithiri kwa mashambulizi ya makombora. Madaktari wa uokoaji wanafunikwa macho na kupigwa risasi. Watoto, wanawake, wazee na waliojeruhiwa wanauawa shahidi kwa kulipuliwa mahema yao. Sera ya njaa ya Amerika, iliyotekelezwa na wafuasi wake, umbile la Kiyahudi, imeongeza mateso hadi kiwango cha baa la njaa. Sasa imedhihirika kwa kila mtu kwamba Firauni wa Washington anafanya maangamizi makubwa kwa Gaza, kwa usaidizi kamili wa kijeshi na uongozi wa kisiasa wa Waislamu na Mayahudi.
Hizb ut Tahrir/Wilayat Tunisia ilifanya kongamano lake la kila mwaka la Khilafah mnamo siku ya Jumamosi, 26 Aprili 2025, katika ukumbi wa mikutano kwenye makao makuu ya Hizb katika makutano ya barabara ya Sakra katika mji mkuu, Tunis, chini ya kichwa: “Kufeli kwa Serikali ya Kisasa na Kutoepukika kwa Dola ya Khilafah” Kumbi mbili zilizotengwa kwa ajili ya wageni zilijaa idadi kubwa ya wanaume na wanawake waliofika kwenye kongamano hilo kutoka pande zote za ardhi ya kijani ya Tunisia.
Kufuatia mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wa Gaza, Hizb ut Tahrir/Kenya mnamo siku ya Ijumaa tarehe 18 Aprili, ilifanya ilifanya kisimamo baada ya Swala ya Jumaa jijini Mombasa na Nairobi. Katika Jiji la Pwani, kisimamo kilifanyika nje ya Masjid Nur huku Nairobi kikifanyika katika Masjid Hidaya mtaa wa Eastleagh. Mada kuu ya Kisimamo ilikuwa ni kuibua wito wa dhati kwa Majeshi katika nchi za Kiislamu kuvunja minyororo ambayo watawala wao wamewaweka katika kambi zao ili wasonge mara moja kuukomboa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa kutoka katika makucha ya Mayahudi wanaoukalia kwa mabavu.
Mnamo tarehe 3 Aprili 2025, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ilitangaza kwamba “inalaani vikali uvamizi unaoendelea na unaozidi kuongezeka wa Israel.” Shirika hilo linajisifu kama “sauti inayounganisha ulimwengu wa Kiislamu.” Lakini watu wa Gaza hawahitaji “sauti,” bali vitendo kutoka kwa majeshi ya Waislamu.
Sisi ni Umma wa watu bilioni mbili, na Pato la Taifa ni $8.7 trilioni na usawa wa nguvu ya ununuzi ya $26.4 trilioni. Tuna akiba kubwa zaidi ya nishati na madini ulimwenguni, na idadi kubwa vijana changamfu. Sehemu inayokosekana ya mlingano huo ni uongozi mnyoofu wa kisiasa, Khilafah Rashida. Swali pekee lililobaki ni: Je, tuko tayari kupambana na kujitahidi kusimamisha dini ya Mwenyezi Mungu ndani ya dola ya Khilafah?
Maoni ya habari yaliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.
Matembezi yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 13 Shawwal al-Khair 1446 H sawia na tarehe 11 Aprili 2025 M kuanzia Msikiti wa Al-Fath kunusuru watu wa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa ulio mateka, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunisia chini ya kichwa: “Gaza Inahitaji Majeshi Kuwapindua Watawala na Kutangaza Jihad”
Enyi Majeshi “Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?”