Jumanne, 08 Rabi' al-thani 1447 | 2025/09/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ametokea kwa Mlango, Anaingia kwa Dirisha

(Imetafsiriwa)

Habari:

Trump asema ‘mambo mabaya’ yatatokea ikiwa Afghanistan haitarudisha kambi ya anga ya Bagram. (Reuters)

Maoni:

Kwa mara nyengine tena, Amerika inafichua kiburi chake mbele ya ulimwengu. Onyo la Donald Trump kwamba “mambo mabaya yatatokea” isipokuwa Afghanistan ikabidhi Kambi ya Anga ya Bagram inaakisi sauti ile ile ya kibeberu ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikifafanua sera ya Marekani kwa ardhi za Waislamu. Maneno kama haya sio lugha ya dola huru zinazoamiliana kwa usawa, bali ni maagizo ya mkoloni ambaye anaziona ardhi za Waislamu kama kituo cha kijeshi kwa ajili ya matamanio yake. Hii ndiyo hali halisi ya siasa za Magharibi: ushurutishaji, vitisho, na kudharau ubwana wa nchi zetu.

Msisitizo wa Marekani juu ya kuiregesha kambi yake nchini Afghanistan unadhihirisha utegemezi wake kwa maeneo ya Waislamu katika kuendeleza nguvu za kijeshi. Bila ngome kama hizo, Amerika haiwezi kudhibiti eneo hilo au kuwadhibiti na mahasimu wake. Bagram haihusiani na usalama wa Afghanistan—inahusu udhibiti wa Marekani, kuhakikisha kwamba Waislamu wanabaki wamegawanyika na kutiishwa huku ardhi na rasilimali zao zikitumikia maslahi ya kigeni.

Jambo lililo wazi ni kwamba huku Amerika ikishindwa kijeshi nchini Afghanistan, haikupata kushindwa kisiasa. Zaidi ya miongo miwili, ilichora ramani ya utajiri wa Afghanistan lakini kwa makusudi iliiacha bila kuimarishwa, na kuhakikisha kwamba Taliban hawakurithi chochote isipokuwa magofu. Badala ya kuungana na Ummah mzima kufuata faradhi ya Kiislamu ya kusimamisha Khilafah, Taliban walijifunga ndani ya mipaka ya kikoloni na kutafuta uhalali kutoka kwa dola zile zile zilizoiharibu nchi hiyo.

Maneno ya Trump leo yanathibitisha uhalisia huu: Amerika haikuondoka kabisa Afghanistan. Badala yake, iliacha dola dhaifu, iliyofungwa pingu—dola ambayo inaweza kuathiriwa na watu wa nje. Kwa kukubali Afghanistan “inahitaji kile tunachotoa” na kwa kuangazia umuhimu wa kimkakati wa Bagram, Washington inaonyesha kuwa ukaliaji wake ilibadilika tu badala ya kumalizika. Hii ndiyo dhati ya sera ya kikoloni—haribu, zuia, na regea wakati wowote maslahi yanapohitaji.

Hili sio tu kuhusu kambi moja ya anga. Inahusu mapambano ya kilimwengu: shauku ya Ummah ya uhuru dhidi ya azma ya Magharibi kudumisha udhibiti. Ni lazima tukatae vitisho hivi vya kiburi na kuelewa kwamba ukombozi wa kweli hautakuja kupitia makubaliano ya kigeni, serikali za vibaraka, au kauli mbiu tupu. Utakuja tu kwa umoja juu ya Uislamu—kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo italinda ardhi zetu na kung’oa kwa uthabiti ushawishi wa kikoloni.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu