Jumanne, 08 Rabi' al-thani 1447 | 2025/09/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  30 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 37
M.  Jumatatu, 22 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Majibu ya Vyombo vya Habari kwa Yaliyomo kwenye Makala ya Mwandishi Sabah Muhammad Al-Hassan

(Imetafsiriwa)

Tumepitia makala ya mwandishi wa habari Sabah Muhammad Al-Hassan kwenye Mtandao wa Sudan Rasd, ya tarehe 22/09/2025, yenye kichwa: “Kwa nini Muungano wa Afrika ulipendekeza mpango sambamba na Quartet licha ya kukaribisha taarifa yake na utayari wa kufanya kazi nao?!”

Ambapo mwandishi huyo alitaja katika hitimisho la makala hayo katika wigo wa mwisho yafuatayo: “Kenya yaainisha rasmi Ikhwan al-Muslim na Hizb ut Tahrir kama makundi ya kigaidi chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi Sura ya 59B, hivyo kuwakilisha hatua muhimu katika juhudi za nchi hiyo kupambana na ugaidi.”

Na kabla ya kujibu aliyoyataja mwandishi kuhusu Hizb ut Tahrir, tunamuuliza: ugaidi ni nini, na je, maelezo hayo yanatekelezeka kwa Hizb ut Tahrir?!

Kwanza: Hakuna ufafanuzi wa ugaidi iliokubaliwa kimataifa ili dola za kikoloni ziutumie kama kitisho kuupiga vita Uislamu, na Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush Mwana alisema wazi wazi baada ya matukio ya 11 Septemba 2001: “Vita hivi vya msalaba, vita hivi dhidi ya ugaidi”, na mwandishi anajua nini maana ya vita vya msalaba. Kuhusu rais wake wa zamani Barack Obama pia alisema: “Kampeni yetu ... hatimaye ni vita ya moyo na akili.” ikimaanisha vita vyao vinavyodaiwa dhidi ya ugaidi. Na la kusikitisha, baadhi ya Waislamu ambao wamedanganyika bila ufahamu hukariri misemo ya ugaidi na magaidi inaotumikia sera ya Makafiri wakoloni wa Magharibi ambayo ni chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Pili: Hatujui ni vipi mwandishi aliingiza mada ya ugaidi, na uainishaji wa Kenya wa Hizb ut Tahrir kama kundi la kigaidi, ingawa mada yake ilikuwa juu ya Muungano wa Afrika na Quartet, isipokuwa kama alikuwa na lengo fulani, na tunataraji kwamba hii sio kweli, kwa sababu Bi Sabah anaijua Hizb ut Tahrir vizuri kwa vile alikuwa akifanya kazi na gazeti la ALJAREEDA ALSUDAIA, na mawasiliano ya Hizb na gazeti hilo, na inajua vyema kwamba Hizb ut Tahrir haitekelezi vitendo vya kisilaha, bali inatekeleza vitendo vya kifikra na kisiasa.

Tatu: Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu, kinataka kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume kwa njia ya kisiasa, na hakitekelezi vitendo vyovyote vya kisilaha si kwa kumwogopa mtu yeyote, bali ni kujifunga na njia ya Mtume (saw) katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu.

Nne: Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilikuwa wazi katika kufichua mipango ya Marekani katika vita hivi vya kipuuzi ambapo Marekani inatafuta kuwaondoa watu wa Uingereza, na kuwaweka watu wake kutoka jeshini katika utawala, kwani pia inataka kuichana Sudan kwa kuitenganisha Darfur kwa hali ile ile ambayo kwayo iliitenganisha Sudan Kusini. Na Hizb imetekeleza na bado inaendelea kutekeleza vitendo vya kisiasa vinavyoonekana ili kuzuia kusambaratika kwa Sudan, kwa hivyo ingekuwa sahihi kwa mwandishi wa habari Sabah, kama alikuwa na shauku juu ya umoja wa nchi, kusitisha vita, na kuzuia mipango ya Amerika ya Kimagharibi, ingekuwa sahihi kwake kutaja taarifa, matoleo, na amali za Hizb angalau kwa pembe ya uadilifu wa habari, na ufikishaji wa habari. Lakini hakuona chochote isipokuwa kile ambacho Kenya ilifanya dhidi ya Hizb ut Tahrir, na hili ni jambo la kimaumbile kwa Kenya na dola nyenginezo ndogo zinazofuata ukoloni, na ambazo zinafuata nyayo zake katika vita dhidi ya Uislamu.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu