Kuweka Matumaini juu ya Kuvunjika kwa Safu za “Israel” ni Usaliti Mpya wa Gaza
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kura moja ya maoni ilifichua kuwa 56% ya “Waisraeli” wanaogopa kusafiri nje ya nchi, 67% wanaamini kuwa serikali haiwawakilishi na 62% wanaunga mkono makubaliano ya kina ya kusitisha mapigano kati ya umbile la Kiyahudi na Hamas, ikiwemo kuachiliwa huru kwa mateka. Tovuti ya “Zman Yisrael,” ambayo ilichapisha maelezo ya kura hiyo ya maoni mnamo tarehe 5 Septemba 2025, ilifafanua kuwa wengi wa “Waisraeli” walionyesha kutokuwa na uwezo wao wa kusafiri nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa ukosoaji wa kimataifa wa umbile lao pamoja na kutengwa kunakoendelea kwa kimataifa kwa dola yao na kuendelea kwa vita mjini Gaza.