- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Si Mtazamaji: Dori ya Marekani katika Shambulizi la ‘Israel’ dhidi ya Doha
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo Septemba 2025, “Israel” ilishambulia Doha, na kuua viongozi wa Hamas na mlinzi wa Qatar. Gazeti la ‘The Independent’ liliripoti kuwa Trump alikasirika kwa sababu Netanyahu alimfahamisha katika dakika za mwisho tu – “He's f***ing me” – huku vyanzo vya “Israel” badala yake vilizungumza kuhusu “idhini” ya Trump. (Independent)
Maoni:
Tofauti na madai ya Trump kwamba hakuwa na ufahamu wa shambulizi la “Israeli” dhidi ya Doha mnamo 9 Septemba 2025, uhusiano wa muda mrefu na ushirikiano kati ya wawili hao unaonyesha kinyume kabisa.
Haiwezekani kabisa kudhani kwamba Washington – pamoja na uwepo wake mkubwa wa kijeshi nchini Qatar na ushirikiano wake wa karibu na “Israeli” – ilikuwa haijui kabisa operesheni kubwa kiasi hiki. Kwa miongo kadhaa, Marekani na “Israel” zimedumisha ushirikiano wa kijeshi na kisiasa ulioimarishwa sana. Chini ya Mkataba wa Maelewano unaoendelea hadi 2028, “Israel” inapokea $ 3.8 bilioni kila mwaka katika msaada wa kijeshi wa Marekani. Nchi hizo mbili kwa pamoja hutengeneza mifumo ya ulinzi wa makombora kama vile Arrow na Iron Dome, hushirikiana pakubwa kijasusi, hufanya mazoezi ya pamoja, na kudumisha ushirikiano wa karibu wa kiteknolojia.
Kwa kuongezea, Qatar ni mwenyeji wa Kambi ya Anga ya Al Udeid, kambi kubwa zaidi ya anga ya Amerika katika Mashariki ya Kati, ambapo maelfu ya wanajeshi wa Marekani wamewekwa na ambapo makao makuu ya CENTCOM yapo. Kambi hii imewekwa mifumo ya hali ya juu zaidi ya rada na ulinzi wa anga. Kwamba shambulizi la kiwango hiki—roketi zilizorushwa kutoka kwa ndege za kivita kwenye Bahari Nyekundu, na kupenya anga ya Qatar—zingeenda bila kutambuliwa sio jambo la kuaminika. Ikiwa mifumo haikuona chochote, basi ujanja wa busara wa aina hii haungewezekana bila ufahamu wa kina wa uwezo wa rada shirikishi. Ikiwa waliona kitu lakini wakashindwa kujibu, inaelekeza kwenye idhini ya kimya kimya.
Maswali pia yanaibuka kuhusu jinsi ndege za “Israel” zingeweza kutekeleza misheni yao bila kutambuliwa na Saudi Arabia, ambayo imetumia mabilioni kwa ajili rada za Amerika na mifumo ya ulinzi ya Patriot. Mifumo hii imeundwa mahsusi kutambua na kuzuia vitisho vya makombora ya balistiki. Kwamba hakuna Qatar wala Saudi Arabia iliyoonyesha hisia yoyote inaimarisha tu hisia ya uratibu, au angalau idhini ya kimya kutoka kwa Washington.
Operesheni ya kiwango hiki kawaida huhitaji ujazaji mafuta wa angani. “Israel” inamiliki ndege zake zenyewe za mafuta, lakini kwa kuzingatia umbali na ugumu, haimkini kabisa kwamba misheni hii ilitekelezwa bila usaidizi wa usaidizi wa kilojistiki wa Marekani.
Netanyahu alijaribu kupanga shambulizi hilo kama ulipizaji kisasi mara moja kwa kifo cha wanajeshi wa “Israel”. Lakini vyanzo vingi vya kuaminika vinathibitisha kwamba operesheni hiyo, iliyopewa jina la Mkutano wa Moto, ilikuwa imeandaliwa kwa miezi kadhaa. Vyombo vya habari vya “Israel” vinazungumza juu ya miezi miwili hadi mitatu ya upangaji, na maandalizi yaliyoimarishwa katika wiki chache kabla ya shambulizi. Misri hata iliripotiwa kuwaonya viongozi wa Hamas mapema kwamba wanaweza kulengwa. Hii inaonyesha wazi halikuwa jibu la ghafla, lakini ni operesheni iliyopangwa kwa muda mrefu.
Taswira hiyo inaongezeka kuwa ngumu zaidi kwa ufafanuzi unaogongana wa dori ya Washington. Kulingana na jarida la ‘The Wall Street’ na ‘The Independent’, Trump alikasirishwa kwamba Netanyahu alimfahamisha muda mfupi tu kabla ya shambulizi hilo—“He’s f***ing me,” iliripotiwa kusema. Walakini vyanzo vya “Israel” vinasisitiza kuwa operesheni hiyo ilifanywa kwa “idhini” ya Trump. Riwaya yoyote ambayo ni kweli, zote zinasisitiza mkorogo wa kina wa Marekani na “Israel” katika ngazi ya juu zaidi ya maamuzi ya kijeshi na kisiasa.
Shambulizi hili pia linaingiliana na mtindo maarufu wa operesheni za “Israel”: wakati wowote fursa za kidiplomasia au mazungumzo ya kusitisha mapigano yanapojitokeza, “Israel” huongeza uhasama kupitia mauaji yanayolenga. Tafakari mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh jijini Tehran mnamo Julai 2024, au mauaji ya Nasrallah jijini Beirut mnamo Septemba 2024. Katika visa vyote viwili, nyakati muhimu za kisiasa zilihujumiwa kimakusudi.
Shambulizi la Doha liliharibu upatanishi wa Qatar. Kadhalika, mnamo Juni 2025, wakati raundi mpya ya mazungumzo ya nyuklia kati ya Marekani na Iran ilipokaribia kufanyika, “Israel” ilianzisha Operesheni ‘Rising Lion’ kwa mashambulizi ya kimakusudi kwenye maeneo ya nyuklia na ya kijeshi ya Iran.
Hitimisho: Marekani Si Mtazamaji, Bali Mshirika.
Kila kitu kinaonyesha kuwa Marekani haikuwa mtazamaji tu bali mshiriki mtekelezaji katika mandhari hii, iwe kupitia uratibu amilifu au kimya cha makusudi. Ukanushaji rasmi unaingiliana na mtindo uliozoeleka wa udanganyifu na unafiki wa serikali na mifumo dhalimu, yenye kiu ya damu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi