Afisi ya Habari
Tanzania
H. 5 Rabi' II 1447 | Na: 1447 / 02 |
M. Jumamosi, 27 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir/ Tanzania Yafanya Dua na Kisimamo
Kutaka Ummah Usiitelekeza Gaza
(Imetafsiriwa)
Jana Ijumaa, tarehe 26 Septemba 2025 M / 04 Rabi' al-Akhir 1447 H baada ya swala ya Ijumaa Hizb ut Tahrir / Tanzania iliandaa kampeni ya nchi nzima kukumbusha Majeshi ya Ulimwengu wa Kiislamu, Wanazuoni wa Kiislamu na Ummah kwa jumla juu ya wajibu wao wa kuiokoa Gaza na kutoitelekeza.
Kampeni hiyo ilijumuisha Dua jijini Dar es Salaam na Zanzibar, ambapo katika Masjid Rahmah, Buguruni Dar es Salaam iliongozwa na Sheikh Mussa Kileo, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano na Masoud Msellem, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania. Dua huko Zanzibar ilifanyika Masjid Mbuyuni, Zanzibar mjini. Pia kulikuwa na visimamo na Khutba za Ijumaa katika maeneo tofauti tofauti nchini Tanzania.
Ujumbe wa kampeni (chini ya taarifa hii kwa vyombo vya habari) uliyahutubia majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu kusonga haraka ili kuingilia kati kijeshi kuikomboa Palestina, Waislamu wa Gaza, Masjid Aqsa na kuling'oa umbile ovu na chafu la Kiyahudi.
Ujumbe huo uliwakumbusha Wanazuoni wa Kiislamu kuwawajibishe na kuwanyoosha watawala vibaraka katika ulimwengu wa Kiislamu, ambao utiifu wao katika kuiunga mkono ‘Israel’ umevuka mipaka.
Pia, ujumbe wa kampeni unauonya Ummah kutoingia katika mtego wa kuwa kimya kwa suala la mauaji ya halaiki ya Gaza, kwa sababu sauti zao huenda zikawalazimisha wanazuoni na Majeshi kulishughulikia suala hili ipasavyo.
Hatimaye, kampeni hiyo iliwakumbusha Waislamu juu ya ufaradhi wa kufanya kazi ya kusimamisha tena dola ya Kiislamu (Khilafah). Kupitia hilo, Uislamu, Waislamu na matukufu yetu yote yatalindwa kikamilifu.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Kuangamizwa kwa Gaza ni Kuangamizwa Kwetu Sote, Umma wa Kiislamu
Huu ni takriban mwaka wa pili tangu umbile la Kiyahudi kuanza mashambulizi yake ya kikatili yaliyoambatana na mauaji ya halaiki mjini Gaza kufuatia tukio la 7 Oktoba 2023.
Uvamizi wa umbile la Kiyahudi kwa amri, msaada wa kijeshi, kisiasa na kidiplomasia kutoka Marekani pia likisaidiwa na nchi kadhaa za Magharibi yamesababisha uharibifu usio na kifani.
Mauaji ya halaiki yamesababisha hasara ya maisha ya Waislamu 65,000 na kujeruhi maelfu, wengi wao wakiwa wanawake na watoto (kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza na vyombo vikuu vya habari vya kimataifa). Vyanzo vyengine vinasema kuwa zaidi ya watu laki mbili wameuawa hadi sasa!
Aidha, uvamizi huo ambao tayari umeharibu karibu eneo lote la Gaza isipokuwa sehemu ndogo ambayo inamalizwa hivi sasa, mbali na kuharibu karibu robo tatu ya majengo ya makaazi, umesababisha uharibifu mkubwa kwa rasilimali watu na miundombinu mbalimbali. Kwa mfano, zaidi ya waandishi wa habari 270 wameuawa, hadi kufikia Agosti 2025 (Chaneli ya Al Jazeera), mamia ya walimu wakiwemo wale wa vyuo vikuu wameuawa, takriban wahudumu wa afya 1400 wameuawa (Mtandao wa Relief), 79% ya misikiti na makanisa matatu yameharibiwa katika Ukanda huo, zaidi ya 255 wasomi wengi wa Kiislamu wameuwawa, na wengine wengi wako kizuizini nk. (Wizara ya Wakfu ya Gaza). Miongoni mwa hospitali 36 za Ukanda wa Gaza, ni chache zinazofanya kazi, huku nyingi zikipigwa mabomu au kuharibiwa nk. Bila kusahau uvamizi unaoendelea wa ‘Israel’ katika Ukingo wa Magharibi ulioambatana na mauaji, ubomoaji wa nyumba, uharibifu wa mashamba, kufukuzwa kwa nguvu, ukamatwaji kiholela, na kadhalika.
Ukandamizaji, ukatili na mauaji yote ya umati yanayofanywa na umbile la Kiyahudi, huku kwa mara ya sita, Marekani ikipiga kura kupinga azimio la usitishaji vita wa Gaza ili kuzuia uvamizi na mauaji ya halaiki. Bila kutaja vitisho vyake kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yote yanayopendelea na kuitetea ‘Israel’ licha ya Tume Huru ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa na baadhi ya taasisi za ndani za haki za binadamu za ‘Israel’ kutangaza waziwazi kuwa umbile hilo linatekeleza mauaji ya halaiki huko Gaza.
Enyi Majeshi katika Ulimwengu wa Kiislamu hususan muliko jirani na umbile la Kiyahudi,
Je, munajua kwa hakika kwamba muna wajibu mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) wa kuiokoa Gaza kwa sababu muna uwezo mikononi mwenu? Je! munajua kwamba nguvu mulizo nazo ni amana kutoka kwa Mola wenu Mlezi ya kuwalinda watu wenu na sio watawala vibaraka? Je, bado munatilia shaka maovu na ukatili wa umbile la Kizayuni? Munasubiri nini kukomboa Gaza? Je, bado munasitasita huku mukiliamini umbile hilo pamoja na yote linaloendelea kuyafanya, akiwemo Waziri Mkuu wao kutamka waziwazi lengo lao la kutwaa ardhi zetu ili kukamilisha mradi wao wa ‘Israel Kubwa’?
Au bado muna matumaini kuwa umbile la Kizayuni lingeleta amani na utulivu huku mukishuhudia kila siku mashambulizi yao dhidi ya Syria, Yemen, Lebanon na hivi karibuni Qatar nk.? Umbile hili haliheshimu ubwana wa nchi yoyote kwa mujibu wa sheria zao za uwongo za kimataifa wala mikataba na makubaliano. Chukueni fursa hii adhimu kuing’oa ‘Israel’ na mumuonyeshe Mwenyezi Mungu (swt) ushujaa wenu wa kweli, ambao hatuna shaka nao, na nyinyi ndio tumaini pekee la Ummah wetu.
Enyi Wapendwa Wanazuoni wa Kiislamu!
Nani atawawajibisha, kuwakosoa, na kuwanyoosha watawala vibaraka katika ulimwengu wa Kiislamu, ambao utiifu wao katika kuunga mkono ‘Israel’ umevuka mipaka ya aibu? Vibaraka hawa wanatumia bandari zao, anga, na rasilimali za Umma wa Kiislamu kuwepesisha na kuiwezesha ‘Israel’ kuendelea kuiangamiza Gaza, na cha ajabu wakati huo huo wakitaka Hamas iwaachilie mateka na kusalimisha silaha zao! Vibaraka hawa wanaunga mkono sera hatari ya ‘suluhisho la dola mbili,’ ambalo ni mtego hatari dhidi ya Umma wa Kiislamu. Suluhisho la mtego ambalo baadhi ya nchi za Magharibi kama Uingereza na Ufaransa zinajifanya kuunga mkono katika ‘kuihurumia’ Palestina ilhali bado wanajificha nyuma yake kwa sababu tangu mwanzo zimekuwa zikishikamana na ‘Israel’ katika ukatili wake.
Pazeni sauti zenu, enyi Wanazuoni, tumieni mimbari zenu na majukwaa mengine kuwakosoa vikali watawala vibaraka waliofikia kiwango cha chini kuliko hata watumwa. Je, hamuoni jinsi Qatar ilivyoibembeleza Marekani kwa kumpa Trump kiasi kikubwa cha fedha na zawadi nyingine za kifahari, kisha Marekani inawapa silaha na idhini umbile la Kiyahudi kuishambulia nchi yao? Je, kuna aibu na udhalilifu mkubwa kuliko huu? Trump na umbile la Kiyahudi wanawachukulia watawala hao vibaraka kuwa waoga hata kwa kufikia kiwango cha paka.
Enyi Wanazuoni wa Ummah!
Haijalishi ni muda gani utapita, musiache wala musichoke kuwasaidia Waislamu wa Gaza kwa sababu wao ni sehemu ya Ummah wetu. Kwa hiyo, watie nguvu askari na Ummah ili kusimama imara na katika kutekeleza majukumu yao kwa Gaza. Msiwasahau Waislamu wa Gaza, angalau kwa dua katika misikiti yenu.
Enyi Umma Mtukufu wa Kiislamu,
Je, hamjui kuwa kimya chenu ni hatari katika mambo kama haya na mifano yake? Mkisimama kidete kwa sauti zenu, mtawalazimisha wanazuoni na Majeshi kushughulikia ipasavyo masuala ya Ummah wenu. Msiingie katika mtego wa shetani kwa kughafilika. Je, mnashindwa na makafiri wanaopaza sauti zao katika kuwatetea watu wa Gaza wakiongozwa tu na ubinadamu pekee, huku nyinyi mna Aqida ya Kiislamu na udugu wa Kiislamu? Sauti zenu ni wajibu wa kuwahimiza wanazuoni na majeshi ya mataifa ya Kiislamu kuchukua hatua.
Kwa kumalizia, yanayotokea Gaza na mateso mengine katika ulimwengu wa Kiislamu ni matokeo ya Ummah wetu kukosa Dola ya Khilafah kulinda na kusimamia mambo ya Ummah wetu ikiwa ni pamoja na kulinda mali, heshima, na damu zetu. Ni wajibu kwa kila Muislamu kufanya kazi ya kusimamisha tena dola ya Khilafah ambayo ni ngao ya kweli kwetu sote.
26 Septemba 2025 M
04 Rabi' al-Akhir 1447 H
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
https://www.hizb-uttahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/tanzania/5017.html#sigProId9f8e5abb3e
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |