Kongamano la Amani ya Kiraia jijini Damascus Utangulizi wa Kuwaondoa Watiifu wa Serikali na Kuhalalisha Nembo za Ukandamizaji na Uhalifu
- Imepeperushwa katika Syria
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na Kamati ya Amani ya Kiraia katika jengo la Wizara ya Habari jijini Damascus mnamo Jumanne, Juni 10, 2025, chini ya uenyekiti wa mwanakamati Hassan Soufan, ulizua wimbi kubwa la hasira na chuki kubwa miongoni mwa Wasyria, hasa miongoni mwa familia za mashahidi na waliopotea, na watoto wa mapinduzi. Wengi waliona kauli za mkutano huo kama uchochezi kwa familia za wahasiriwa, kupuuza mihanga ya wanamapinduzi, kudharau damu ya mahsahidi, kukana ukweli usiopingika, na uhalalishaji wa wazi wa wahalifu wa kivita. Hafla hiyo ilionekana kama jaribio la kulalalisha mahusiano kwa nembo za utawala ulio ng’atuliwa chini ya mabango ya "amani ya raia," "kujenga taifa," na "kuzuia umwagaji damu."