Alhamisi, 03 Sha'aban 1447 | 2026/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Rajab 1447 Na: HTS 1447 / 84
M.  Jumamosi, 17 Januari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mapendekezo ya Kongamano Lililofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Kukumbuka 105 Hijri Tangu Kuvunjwa kwa Khilafah
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumamosi, tarehe 28 Rajab 1447 H, sambamba na tarehe 17 Januari 2026 M, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya kongamano la kumbukumbu ya miaka 105 tangu kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu ya Khilafah. Kongamano hilo lilihudhuriwa na watu mashuhuri, wakiwemo wanasiasa, watu mashuhuri wa vyombo vya habari, wasomi, na viongozi wa jamii. Kwa kuzingatia kwamba kumbukumbu hii chungu inakuja huku sisi nchini Sudan tukiteseka kutokana na vita vilivyowashwa na ubeberu wa Marekani, ikiwatumia vibaraka wake wa ndani kusambaratisha kile kilichobaki cha umoja wa nchi yetu chini ya sera yake inayoitwa “Mipaka ya Damu”. Hivyo, kichwa cha kongamano letu kilikuwa: “Sudan Kati ya Sera za Mipaka ya Damu na Kuunganisha Watu Kuwa Umma Mmoja.” Kongamano lilianza kwa hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde, kisha wazungumzaji kutoka kwa wabebaji wa Dawah walijadili kuingia kwa Uislamu nchini Sudan, na jinsi ilivyokuwa sababu ya umoja wa Waislamu na kukusanyika kwao, kisha kuingia kwa ukoloni wa Uingereza na jinsi ulivyoshambulia misingi ya umoja, kufuatia sera ya gawanya utawale. Kisha nchi hii ilibadilishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia kuwa uwanja wa mzozo wa kimataifa kati ya ukoloni wa Uingereza na Marekani, na bado ingali hivyo, hadi mzozo kati yao ukawa mauaji mabaya ya kijeshi, ukilenga usalama wa watu wa Sudan, matukufu yao na umoja wa nchi yao, ambao uliifanya Amerika kutangaza waziwazi sera yake inayolenga kuzichana nchi za Waislamu, na kuchora nchi mpya ndani yake zenye mipaka iliyochorwa kwa damu ya Waislamu. Kisha nyaraka za kongamano zilizungumzia kuhusu sera ya kuwayeyusha watu kuwa umma mmoja, ambayo haijafanikiwa katika historia ya mwanadamu kujitokeza isipokuwa kwa dola ya Waislamu, Khilafah, na haja ya watu leo, katika kumbukumbu ya kuvunjwa kwake, kuharakisha hatua na kuharakisha mwendo ili kuiregesha kwa njia ya Utume.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunawahutubia watu wetu wote, haswa viongozi wao, wanazuoni, na watu wenye ushawishi—wanasiasa, waandishi, na wanahabari—kukubaliana nasi kwamba Dini yetu tukufu inatuwajibisha kufanya yafuatayo:

Kwanza: Kuufanya Uislamu pekee kuwa ndio msingi wa maisha yetu na suluhisho la matatizo yetu. Hili linahitaji kung'oa ushawishi wa makafiri, Magharibi ya kikoloni, haswa Amerika na udhibiti wake juu yetu. Hili linaweza kupatikana tu kupitia Uislamu, unaotekelezwa na Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume.

Pili: Kulifanya fungamano linayotuunganisha kuwa udugu wa Uislamu na si chengine chochote. Haipaswi kuzingatia mafungano ya kizalendo, kabila, kijamii, au eneo, kwa sababu haya yote yanagawanya badala ya kuunganisha. Lazima tukatae wito wowote unaotokana na mafungamano haya machafu, hasa kutokana na kuongezeka kwa mzozo wa kikanda na kikabila, ambao unatumikia ajenda ya mipaka ya damu.

Tatu: Lazima tuwang'oe farasi wawili wa Trojan wa Magharibi mkoloni kafiri katika nchi yetu: Utawala wa Kiraia na mfumo wa Hawakir. Ama kuhusu Utawala wa Kiraia, umekuwa, kama wakoloni wa Uingereza walivyokusudia walipouunda, tishio kwa umoja wa nchi. Kuhusu fikra ya Hawakir, ambayo wanaitegemea kwenye ramani zilizochorwa na wakoloni wa Uingereza, inamaanisha kutoa umiliki wa ardhi, pamoja na vichaka vyake, misitu, na malisho, kwa kabila moja katika eneo kwa kuwatenga makundi mengine, na kuifanya hii kuwa sababu ya migogoro. Hili ni haramu kwa sababu, kulingana na sheria ya Kiislamu, ardhi ya Sudan ni ya Kharaj (kodi ya ardhi), na umiliki wake ni wa Hazina ya Dola ya Waislamu (Bayt al-Mal). Raia yeyote wa serikali anaweza kumiliki matumizi yake kwa ajili ya makaazi, kilimo, au madhumuni mengine yoyote. Kuhusu malisho, vichaka, na misitu, ni mali ya umma, ikimaanisha kuwa ni ya watu wote, kama Mtume (saw) alivyosema: «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ، فِي الْكَلَأِ، وَالْمَاءِ، وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika mambo matatu: malisho, maji, na moto.

Nne: Vikosi vya jeshi vya dola ni kikosi kimoja, chenye umoja, ikiwemo polisi. Kuwepo kwa wanamgambo na maumbo mengine yenye silaha hakuruhusiwi, kwani uwepo wao ni tishio kwa hadhi ya dola. Hii ni kwa sababu nguvu hukaa na kundi lenye nguvu zaidi ndani ya dola, na wingi wa vikundi hivyo ni ishara ya mzozo na mgawanyiko wa dola, hasa kutokana na urahisi ambao maumbo haya yanaweza kupenywa na maadui wa nje.

Tano: Tunapaswa kujitahidi kusimamisha dola inayotuunganisha, inayotuletea heshima, na inayomridhisha Mola wetu Mlezi, yaani, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo Mtume (saw) aliitoa bishara njema kwamba itakuja baada ya utawala dhalimu ambao siku zake za mwisho tunaishi ndani yake, Mwenyezi Mungu Akipenda, akasema: «... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ يَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا اللهُ إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ» “...kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa atakapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha akanyamaza.”

Sita: Jambo la kiburi cha Trump na majivuno yake kupita kiasi, uonevu wake kwa mataifa ya dunia, uharibifu wake wa sheria za kimataifa ambazo uongozi wa nchi yake ulizijumuisha hapo awali, na kutoweza kwa dola za kitaifa kumpinga, yote haya yanazungumzia haja ya dunia ya dola iliyojengwa juu ya msingi wa Uislamu; Khilafah kwa njia ya Utume, ili kuuondolea ulimwengu maovu ya Ubepari na uongozi wa Amerika.

Kwa kumalizia: Ujumbe kwa waumini wenye ikhlasi kwa itikadi yao miongoni mwa watu wenye nguvu na ulinzi nchini Sudan, kwa wale wanaosukumwa na itikadi tukufu ya Uislamu, kwa wahudhuriaji wa misikiti wanaohudhuria swala za Ijumaa na swala za jamaa, na wanaomwogopa na kumcha Mwenyezi Mungu: Jueni kwamba hali imefikia hatua muhimu, na watu wenu wanakuombeni msaada dhidi ya chuki ya Magharibi kafiri na zana zake ambao hawajali agano au wajibu wowote. Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt) kwenu na hukmu zake yanaweka uthibitisho dhidi yenu, na ukweli wa kikanda na kimataifa unakuandaeni na kukuiteni kumtii Mwenyezi Mungu. Aqida (itikadi) ya Uislamu, pamoja na ukweli wake, zinakulindeni kutokana na kurudi nyuma na kumwogopa yeyote ila Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu Zote, Mwenye Uweza, Mwenye mamlaka na nguvu. Yote haya yanakuombeni muinusuru Hizb ut Tahrir ili iweze kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili iweze kuweka dira ya sayari hii ya Dunia kuelekea maisha ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu, kuwanusuru wanaodhulumiwa na kuwatoa watu kutoka kwenye giza la ukafiri na kuwaingiza kwenye nuru ya Uislamu. Kuweni kama kiongozi wa Ansari, Sa'd ibn Mu'adh, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ambaye kifo chake kilitikisa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, Mwenye Rehema, kwani kuwaiga watu hao ni mafanikio, na kwa kitendo kama hicho na wajitahidi wenye kufanya kazi.

[وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَداً ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]

“Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” [At-Tawba: 100]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu