Ndoto ya Kikoloni ya ‘Dola Mbili’ kwa Palestina
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wakati Gaza ikiendelea kuungua, huku makumi ya watu wakiuawa katika Ukanda huo kila siku, huku wakaazi wake wakiendelea kufa kwa njaa, na wakati ghasia zikiongezeka katika Ukingo wa Magharibi mikononi mwa uvamizi wa kinyama wa Kizayuni, kumekuwa na msukumo mpya, hasa wa baadhi ya nchi za Magharibi, kwa ajili ya ‘Suluhisho la Dola Mbili’ kwa Palestina ambayo wanatoa hoja kuwa litaweza kutatua mzozo wa muda mrefu katika eneo hilo. Ufaransa, Uingereza na Canada miongoni mwa mataifa mengine zimetangaza nia yao ya kuitambua dola ya Palestina, ikiwa masharti maalum yatatimizwa.