Ijumaa, 20 Rajab 1447 | 2026/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  12 Rajab 1447 Na: H 1447 / 040
M.  Alhamisi, 01 Januari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 105, Tunaufufua Wito kwa Majeshi Yote ya Ummah Kuhamasisha Nguvu Zao Ili Kusimamisha Khilafah Rashida
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na tarehe 3 Machi, 1924 M, amri ovu ilitolewa na lile lililoitwa Bunge Kuu la Kitaifa, ikielezea kufutwa rasmi kwa Khilafah. Kwa kuvunjwa kwa Khilafah, hukmu za Sharia ziliondolewa, kiapo cha utiifu (Bay’ah) kilisitishwa, na ardhi za Waislamu zilichanwa vipande vipande kwa misingi ya kitaifa na kikabila kuwa vijidola tete, tegemezi, na dhaifu. Vibaraka wa kulipwa waliteuliwa kuzitawala. Fikra ya umoja ilipigwa pigo kubwa. Kwa kuangamia kwake, Bayt al-Maqdis na Ardhi Iliyobarikiwa zilianguka, na umbile lenye saratani la Kiyahudi lilipandwa katikati ya ardhi za Waislamu.

Umma wa Kiislamu, tangu siku hiyo ya giza na katika kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, bado unaishi katika hali ile ile ya uchungu katika miaka hii yote dhaifu. Mgongano wa hadhara unaofanyika Palestina, kati ya makafiri, Magharibi ya kikoloni, wanaojaribu kuzuia kuanguka kwa umbile la Kiyahudi, na utashi wa Umma wa Kiislamu, ambao unakataa kuiachilia ardhi iliyobarikiwa, bado ni ushuhuda kwa wote, karibu na mbali. Mauaji ya kikatili hayajakoma wala vita vya kikoloni havijapungua. Misiba na dhiki vinauzunguka Umma wa Kiislamu kote ulimwenguni. Mabaniani wanawashambulia Waislamu kwa mauaji na uchinjaji, na nchini China watu wote wamefungwa kwa sababu ni Waislamu, huku ardhi za Waislamu zikizama katika vita visivyo na maana, vikizichana!

Mataifa yote ya dunia yameungana kuupiga vita Uislamu na kurudi kwa Khilafah, hasa kwa kuwa kutajwa kwake kumekuwa jambo la kawaida, kati ya watu, hata midomoni mwa maadui waovu wa Uislamu na Waislamu, ambao wamesibiwa na fedheha na udhalifu. Kila mtu anafahamu kwamba Khilafah ni mradi unaokuja wa mabadiliko, Mwenyezi Mungu akipenda. Ni kutokana na ukubwa wake, itakaporegeshwa, itaachilia nguvu za Ummah na kuuwezesha kuregelea tena dori yake duniani, na kuwa wokovu wa ulimwengu huu kutoka katika hali yake ya sasa. Wamagharibi makafiri wanajua kikamilifu kwamba hawawezi kuzima nguvu za Ummah kama umbo moja, lililo hai lenye imani thabiti.

Viongozi wa ukafiri duniani wanaogopa kurudi kwa Khilafah. Kwa hivyo, ni lazima tutambue kwamba kuungana tena kwa Ummah wa Kiislamu na Dola yake kutakuwa tukio kama mlipuko mkubwa wa nyuklia katika historia ya wanadamu, kwa sababu Dola ndiyo nguvu ya utendaji yenye tija. Kwa kuwepo kwake, vikosi vya Ummah hupangiliwa, nguvu zake huachiliwa, na uwezo wake uliotawanyika unaelekezwa, na kuubadilisha kuwa nguvu yenye tija. Kwa kutokuwepo kwake, Ummah unaanguka na rasilimali zake zinaporwa.

Kwa sababu hii, tunaulingani Ummah wa Kiislamu, pamoja na watu wake, wasomi, majeshi, na wale wenye nguvu na ulinzi, kuharakisha kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili tuweze kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt), kwani ni taji la faradhi zote na ushindi ulioahidiwa.

Tunarudia wito wetu kwa vikosi vyote vya Ummah kuhamasisha nguvu zao kurudi kwenye izza na heshima kubwa iliyokuwepo chini ya Khilafah na utawala wa Sharia safi.

Hizb ut Tahrir imeelezea njia ya kurudi kwenye neema hii kubwa na inaendelea kufanya kazi pamoja na Ummah ili kuukomboa kutoka kwa utiifu kwa mifumo ya ukafiri iliyotengenezwa na wanadamu iliyowekwa na makafiri, Magharibi ya kikoloni, na kuufufua ili uweze kupata tena heshima yake, kukomboa maeneo yake matakatifu, na kuwatoa wanadamu kutoka kwenye giza na dhuluma ya ubepari hadi kwenye haki na rehema ya Uislamu. Kutoka kwa Ubay bin Kaab (ra) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «بَشِّرْ هذهِ الأُمَّةَ بِالسَّنَاءِ والدِّينِ والرِّفْعَةِ والنَّصْرِ والتَّمْكِينِ فِي الأَرضِ، فمَن عملَ منهُم عَمَلَ الآخرةِ للدُّنيا لم يَكُن لَهُ فِي الآخرةِ مِن نَصيبٍ» “Upe Ummah huu bishara njema ya izza, Dini, kunyanyuliwa, ushindi na tamkini juu ya ardhi. Yeyote miongoni mwao na atakayefanya amali ya Akhera kwa ajili ya dunia haitakuwa na hisa katika Akhera” [Musnad ya Imam Ahmad]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-uttahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-uttahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu