Ijumaa, 18 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tamasha la OIC Lahitimisha kwamba Qatar na Dola za Kiarabu Zisalie Waaminifu kwa Kuwa Kiatu Kilicho Chakaa cha Amerika Huku Zikibweka Vikali Mawinguni

Kufuatia shambulizi la kombora la umbile la Kizayuni dhidi ya wanachama wa Hamas nchini Qatar, taarifa ya mwisho ya mkutano wa dharura wa kilele wa Waarabu-Waislamu (OIC na Ligi ya Waarabu) uliofanyika jijini Doha mnamo 15 Septemba 2025, “unashutumu vikali uvamizi wa Israel dhidi ya Qatar, na kuutaja kuwa ni kama pigo kwa matarajio yoyote ya amani katika eneo hilo. Tangazo hilo zilizisihi nchi wanachama kuzingatia upya mafungamano yao ya kidiplomasia na kiuchumi na Israel na kufuata hatua za kisheria dhidi yake.”

Soma zaidi...

Trump, Msaidizi Mkuu wa Umbile la Kiyahudi katika Uhalifu wake wa Kinyama mjini Gaza na Palestina Yote, Anatoa Suluhisho la Maangamivu kwa Gaza, Hata Kulilazimisha, Juu ya Kundi la Watawala katika Nchi za Waislamu!!

Trump alisema katika chapisho kwenye jukwaa lake la Kijamii la Ukweli: “Ninafuraha kuripoti kwamba tuna mazungumzo yenye msukumo na yenye natija na Jumuiya ya Mashariki ya Kati kuhusu Gaza,” na kuongeza kuwa, “mazungumzo makali yamekuwa yakiendelea kwa siku nne, na yataendelea kwa muda mrefu iwezekanavyo ili kupata Makubaliano Yanayokamilishwa kwa Mafanikio.” (Truth Social; TRT Kiarabu, 27/9/2025)

Soma zaidi...

Makubaliano ya Aibu ya Kuhalalisha Usalama na Mayahudi na Miradi ya Ugawaji ni Hatari Kubwa Inayolenga Kuvunja Utashi wa Kiota na Ushindi Uliopata

Katika taarifa ambazo, kusema kwa uchache, ni hatari, zilizotolewa na mkuu wa awamu ya mpito, Ahmed al-Sharaa, vipengee vya hali ya sasa ya Syria vilifichuliwa. Alionyesha kwamba “Syria inajua jinsi ya kupigana, lakini haitaki tena vita,” na kwamba “haina chaguo ila kufikia makubaliano ya usalama na Israel,” wakati “kujitolea kwa Israel kwa makubaliano haya ni suala tofauti.” Pia alieleza kuwa matukio ya Sweida yalikuwa tu “mtego uliotayarishwa makhsusi kuzuia makubaliano ya awali juu ya utaratibu wa usalama,” na kwamba “baadhi ya mirengo ndani ya SDF na PKK ilivuruga makubaliano ya Machi na kupunguza kasi ya mchakato huo.” Amesisitiza kuwa “hali ya kaskazini mashariki mwa Syria inatishia usalama wa kitaifa wa Uturuki pamoja na Iraq,” na akadokeza kuwa “ikiwa uwiano hautafikiwa ifikapo Disemba, Uturuki inaweza kuchukua hatua za kijeshi.”

Soma zaidi...

Makongamano Yenye Malengo ya Kufuta Kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa Yanafanyika Wakati Damu ya Watu wake Ikimalizwa

Milipuko ya mabomu inateketeza miili ya watoto mjini Gaza, njaa inatafuna mabaki yao, mizinga inasaga saga uhai na nyumba za watu walio na msimamo thabiti, na ndege zinanyesheza lava zao kwenye hospitali na hema za waliohamishwa. Kutokana na hali ya uhalifu huu, kongamano lililokongamana jana usiku, 22 Septemba 2025, jijini New York, lililoitishwa na Ufaransa na Saudi Arabia, lilitaka kutambuliwa kwa “Dola ya Palestina”.

Soma zaidi...

Maradhi ya Mkurupuko Yawaangamiza Watu kwa Kukosekana kwa Dola ya Ustawi

Maradhi matatu ya kimazingira—kipindupindu, homa ya dengue, na malaria—yanawaangamiza watu katika majimbo ya Khartoum, Al-Jazirah, na Darfur, katikati ya uzembe wa kutisha na aibu ya kukosekana kwa serikali inayojiita “Serikali ya Matumaini”! Kuna matumaini aina gani wakati watu wanaishi katika mazingira yasiyostahili hata kwa wanyama—mazingira yanayotawaliwa na waenezaji magonjwa, ikiwemo mbu wa malaria, mbu wa dengue, na nzi?

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria Kikao cha Kisiasa

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan inafuraha kuwaalika wanahabari, wanasiasa, na wale wote wanaopenda masuala ya umma, kuhudhuria na kushiriki katika kikao kipya cha Kisiasa, ambapo Ustadh Ya‘qub Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, atakuwa mgeni, chini ya kichwa: Ulaya na Ushawishi Wake kwa Matukio nchini Sudan.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu