Pindi Milango Inapofungiwa wenye Njaa na Kunusuriwa Kukanyimwa, Sura Hasiri ya Serikali ya Misri na Wapambe wake Inafichuliwa
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika wakati ambapo Gaza inastahamili moja ya nyakati kandamizi na za kikatili zaidi katika historia, ambapo, pamoja na kuuawa kwa mashambulizi ya mabomu, watoto wanakufa kwa njaa, wanawake kwa huzuni, na wazee kwa magonjwa, Meja Jenerali Khaled Mewaghar, Gavana wa Sinai Kaskazini, alitoa matamshi ambayo yanakinzana na matakwa rahisi zaidi ya maadili ya kiakhlaki na ya kibinadamu matakwa ya udugu wa Kiislamu. Alisema: “Ikiwa watu wa Gaza watafikia kiwango fulani cha njaa, wana chaguzi tatu: ima kwenda upande wa Israel na kukabili milio ya risasi, kujitupa baharini, au kuelekea Misri—jambo ambalo haliwezekani.”