Jumatano, 04 Rajab 1447 | 2025/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  1 Rajab 1447 Na: H 1447 / 19
M.  Jumapili, 21 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kipindi cha Tarique Rahman: Purukushani ya Kisiasa Kutoka kwa Mfumo wa Kisekula Uliovunjika

(Imetafsiriwa)

Huku Bangladesh ikiingia katika awamu muhimu ya kabla ya uchaguzi, kutangazwa kwa kurudi kwa Tarique Rahman, mwana wa Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh Khaleda Zia na kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Kizalendo cha Bangladesh (BNP), kumesababisha wimbi linalotabirika la umaarufu inaozingatia shakhsiya ya mtu. Simulizi hii, iliyokuzwa kwa ukali na chama chake, inamwakilisha kama suluhisho la pekee kwa changamoto za taifa. Lazima tuone hili kwa jinsi lilivyo: udanganyifu mkubwa wa kisiasa ambao unaficha kwa hatari uhalisia msingi wa mamlaka na mfumo wa leo.

Hadithi ya ngano ya Kufeli kwa Kunakorudiwa ya “Uokozi wa Mtu Mmoja”: Historia, duniani kote na nchini Bangladesh, mara kwa mara hutupilia mbali hadithi ya kiongozi wa kimasihi. Angalia Mapinduzi ya Kiarabu: viongozi walianguka, lakini miundo ya mamlaka inayoungwa mkono na Magharibi ilibaki vile vile. Katika historia yetu wenyewe, kile kilichoonekana kama ‘mabadiliko’ yanayoendeshwa na Dkt. Yunus pekee kiliendeshwa na usaidizi kutoka kwa jeshi, asasi za kiraia, na maslahi ya kigeni. Hakuna kiongozi anayefanya kazi ndani ya ombwe. Msisimko unaomzunguka Bw. Rahman kama “mwokozi” ni udanganyifu hatari. Mabadiliko halisi hayatatoka kwa mtu mmoja, bali kutoka kwa harakati pana inayoweza kupata utiifu wa vituo vilevile vya mamlaka vinavyounga mkono mfumo wa sasa.

Mifumo ndio Hutawala, Sio Shakhsiya za Watu: Kuzingatia shakhsiya ya Bw. Rahman kwa kimakusudi hugeuza umakini kutoka kwa mfumo uliojikita anaowakilisha. Kuanguka kwa madikteta kama Suharto nchini Indonesia au Marcos nchini Ufilipino hakukuwa vitendo rahisi vya ubadilishaji wa kishujaa; yalikuwa ni matokeo ya shinikizo la kimfumo, migawanyiko ya ndani, na mabadiliko ndani ya mfumo wa kimataifa ambayo yaliondoa uungwaji mkono. Mishini ya taasisi za fedha za ukoloni mamboleo (Benki ya Dunia na IMF) na diplomasia ni kigezo kikubwa zaidi kuliko mtu yeyote. Kumpa umaarufu mtu ni mbinu ya kuficha umbile lisilobadilika la mfumo wa kisiasa na kiuchumi unaoungwa mkono na Magharibi ambao chama chochote kikubwa, ikiwemo BNP, lazima kiifuate ili kupata madaraka.

Jiometri Isiyoepukika ya Nguvu ya Dunia: Bangladesh ina thamani kubwa ya kimkakati na kiuchumi. Hakuna mpito wa kisiasa unaowezekana katika ngazi ya kitaifa unaotokea bila kiwango fulani cha ufahamu pamoja na dola kubwa za kimataifa, haswa Marekani na Uingereza, ambazo zina maslahi katika utulivu wa kikanda, biashara, na ushawishi wa kimkakati. Wazo kwamba Bw. Rahman au mtu yeyote wa upinzani anaweza kupanda bila ushiriki huo ni la kijinga. Ikiwa anapewa umaarufu, inaashiria manufaa yanayoonekana na watu wa nje yanayoendana na maslahi yao, sio nguvu huru na ya kuleta mabadiliko kwa Bangladesh.

Ubabaishaji Stahiki Kutoka kwa Kufilisika Kisiasa: Shangwe zinazozunguka kurudi huku kimsingi zinatumika kuficha mapungufu makubwa ya BNP. Inazua swali muhimu: ruwaza ya kuvutia ya chama, mpangilio wake wa mashinani, au njia badali zake halisi za sera ziko wapi? Umma hauoni ila mzunguko wa ubadilishaji wa kipote cha mabepari —ubadilishaji wa seti moja ya watendaji ndani ya mfumo huo huo kwa nyengine, unaoahidi mabadiliko lakini ukiendeleza mienendo ile ile. “Kurudi kwa shujaa” ni udanganyifu wa kisanii, unaopotoa nishati ya umma kutokana na kudai mabadiliko halisi.

Enyi watu, mabadiliko halisi, ya kudumu kwa Bangladesh kamwe hayatafika kwenye ndege hata moja kutoka London. Yataundwa sio kwa kuwatukuza watu binafsi, bali kwa kukabiliana na kung'oa nguzo za kiserikali za mfumo wa leo wa dunia unaoungwa mkono na Magharibi unaoendeleza hali halisi nchini Bangladesh. Na kumkazia fikra mtu ni kuangukia kwenye purukushani hatari hivi sasa.

Uongozi wa dhati wa Hizb ut Tahrir unafanya kazi kwa ajili ya mabadiliko kamili ya mfumo badala ya kubadilisha barakoa ya mfumo uliooza wa kisekula wa kibepari. Kazi ngumu, isiyo na hadhi ya kujenga uwezo halisi kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa kuanzia mwanzo inasalia kuwa njia pekee ya kweli ya kusonga mbele. Kwa hivyo tunawaomba wanasiasa wenye ikhlasi hasa na watu kwa jumla kukusanyika pambizoni mwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kubadilisha mfumo, badala ya kuwa sehemu au watoaji tu wa sarakasi ya kisiasa ya magharibi.

[إِنَّ اللَّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Ar-Ra’d: 11]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu