Jumanne, 03 Rajab 1447 | 2025/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Jumada II 1447 Na: HTS 1447 / 68
M.  Ijumaa, 19 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vyombo vya Usalama Vyawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa Kutoa Wito wa Kutibua Mpango wa Amerika wa Kutenganisha Darfur
(Imetafsiriwa)

Kikosi kutoka kwa vyombo vya usalama kiliwakamata Mashababu watano (wanachama) wa Hizb ut Tahrir katika mji wa Al-Shawak, ambao ni: Othman Al-Amin Kanda, Hassan Al-Amin Kanda, Muhammad Thamin Adam, Ahmad Babikr, na Al-Amin Abdullah. Hili lilikuja kufuatia Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kufanya kisimamo mbele ya Msikiti wa Kale huko Al-Shawak, ambapo Sheikh Othman Al-Amin Kanda, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alihutubia hudhuri ya watu mashuhuri wa eneo hilo na umma kwa jumla. Katika hotuba yake, alielezea hatari ya mpango wa Marekani unaotaka kuigawanya Sudan kwa kuikata Darfur, akiwapa wale waliohudhuria jukumu la Kisharia linalofanya umoja wa Ummah na umoja wa dola kuwa suala nyeti. Baadhi ya watu mashuhuri walishiriki kwa kutoa kauli zinazothibitisha msimamo wao na pamoja na hizb ili kuzuia mpango wa kujitenga.

Wanachama wa Hizb waliinua, wakati wa kisimamo chao, mabango ambayo yaliandikwa:

• Tibueni mpango wa Amerika wa kutenganisha Darfur

• Tibueni mpango wa mipaka ya damu na zuieni kukatwa kwa Darfur

• Simamisheni Khilafah ili kung'oa ushawishi wa Magharibi kafiri kutoka kwa ardhi zenu... na misemo mengine inayohusiana na mada hiyo.

Tabia hii ya vyombo vya usalama inathibitisha kwamba serikali inaendelea na utekelezaji wa mpango wa Amerika unaotaka kuigawanya Sudan kwa kuigawanya Darfur, baada ya kutenganisha kusini mwake kwa njia ile ile inayotumika sasa. Vyenginevyo, wale wanaotaka kuhifadhi umoja wa nchi na kuzuia kuvunjika kwa umoja wake wanawezaje kukamatwa?!

Asili ni kwamba watu kama hawa wanapaswa kuheshimiwa, sio kukamatwa, kwa sababu walitekeleza wajibu wa Sharia ambao watu wengi wa nchi hii—iwe wanajeshi au raia—walishindwa kuutekeleza.

Hakika, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunaiambia mamlaka na vyombo vyake vya usalama: kukamatwa na kunyamazishwa midomo hakutatuzuia kusema ukweli na kuutenda, hata kama gharama ni maisha yetu na damu yetu. Lakini tunawaambia: Mcheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ummah, Mcheni Mwenyezi Mungu kuhusu wabebaji wa dawah, na jueni kwamba hamwezi kumzuia Mwenyezi Mungu.

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]

Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Al-Shu‘ara:227]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu