Kashmir Haiwezi Kukombolewa Bila Kubadilisha Uongozi Unaopoteza Fursa ya Dhahabu ya Kuikomboa Kashmir, kwa ajili ya Kumfurahisha Trump
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Leo, tarehe 5 Agosti 2025, miaka sita imepita tangu kuunganishwa kwa lazima kwa Kashmir Inayokaliwa kimabavu na Raja Dahir wa zama hizi, Modi. Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa nchini Marekani, kuisalimisha Kashmir ilikuwa ni usaliti wa wazi wa uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan wa wakati huo, serikali ya Bajwa-Imran. Miezi michache tu baadaye, Jenerali Bajwa aliendeleza usaliti huu kwa kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano, na Dola ya Kibaniani kuhusiana na Kashmir. Hata hivyo, usaliti huu dhidi ya Waislamu wanaodhulumiwa na wanyonge wa Kashmir uliendelea hata zaidi ya hapo.