Mustakabali wa Vita vya Kisasa na Dori Iliyokosekana ya Khilafah
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vita vinavyoendelea katika sehemu mbalimbali za dunia—hasa vita kati ya Urusi na Ukraine na mzozo kati ya Iran na umbile la Kiyahudi—vinaonyesha wazi kwamba ulimwengu umeingia katika awamu mpya na tofauti ya vita vya kijeshi na kijasusi. Mtazamo wa kale wa vita, uliopitwa na wakati, unaojengwa juu ya vikosi vikubwa vya askari wachanga, vifaru, na mizinga, unabadilika kwa kasi na kuporomoka. Leo, dola kama vile Marekani, China na Urusi zinatenga bajeti kubwa kwa viwanda vya juu vya kijeshi na zinafafanua upya mbinu mpya za kivita. Vita kwenye mstari wa mbele wa kisasa havikomei tena kwa risasi na bunduki – ni vita vya operesheni za kimahesabu (algorithms), akili ya bandia, droni, mtandao na mawimbi ya satelaiti.