- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Uzbekistan iko katika Hali Tete!
Na: Ustadh Ahmad Hadi
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Al-Rayah - Toleo 570 - 22/10/2025
Uchumi wa Uzbekistan uliporomoka baada ya kuvunjika kwa Muungano wa Kisovieti na uhuru wake. Mamilioni ya Wauzbeki waliondoka nchini mwao kutafuta kazi, hasa Urusi, ambapo wakawa wafanyikazi wahamiaji, na wakabaki kwa miaka mingi. Dola hii ilishindwa kuwapa fursa za kazi, au kurekebisha uchumi. Ilishindwa kujenga viwanda na mitambo mipya, na badala yake ikabomoa vile vilivyokuwepo tangu enzi ya Usovieti.
Serikali ilitegemea mikopo na uwekezaji wa kigeni ili kufidia gharama zake, na ikaanza kupata mikopo mingi kutoka Urusi, Muungano wa Ulaya, China, na Marekani. Maafisa walishindana kupata uwekezaji na mikopo hii kupitia njia mbalimbali, huku watu wakiachwa wajitunze bila usaidizi wa serikali.
Nchi zilizotoa mikopo na kuleta uwekezaji kutoka nje zilianza kuweka masharti yao na miongozo ya kisheria, zikitafuta kupanua ushawishi wao nchini. Kimaumbile, Urusi imedumisha ushawishi wake wa awali, ikiuongeza kupitia shinikizo jipya, kama vile vitisho vya kuwafukuza wafanyikazi wahamiaji na kuchochea migogoro ya kiuchumi katika eneo hilo.
Chini ya utawala wa Rais wa zamani wa Uzbekistan Islam Karimov, hadi 2016, deni la nje la nchi hiyo lilifikia dolari bilioni sita. Leo, mwaka wa 2025, deni hili limeongezeka hadi dolari bilioni 72, ambazo nyingi zinatoka China. China imeizidi Urusi kwa kiasi cha uwekezaji na mikopo iliyotolewa kwa Uzbekistan.
Kila dola miongoni mwa dola zinazotoa mikopo na uwekezaji, iwe Urusi, China, Muungano wa Ulaya, au Marekani, inafafanua kwanza kabisa kuzuia kurudi kwa Uislamu ndani ya jamii. Kwa kila uwekezaji au mkopo, na kila mkutano wa kisiasa ndani ya mashirika kama vile Shirika la Shanghai au Ushirikiano wa Eurasia, hufuatiwa na ongezeko la upigaji vita Uislamu na kueneza sera zinazoupinga.
Kwa mfano, baada ya mkutano wa mwisho wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai, mamlaka katika Mkoa wa Namangan, Uzbekistan, ziliwaita wake wa zaidi ya Maimamu 30 wa misikiti kwenye afisi ya mwendesha mashtaka na kuwalazimisha kuvua hijabu zao, wakitishia kuwafuta kazi waume zao, ikiwa hawangefanya hivyo. Vile vile, kampeni dhidi ya khimar na ndevu mitaani ziliongezeka, na serikali ikachukua mbinu ya ufuatiliaji ya China, ikiweka kamera za ufuatiliaji, zilizoagizwa kutoka China katika kila barabara na mahali, ili kutambua nyuso za Waislamu na kuwafuatilia. Wakati huo huo, adhabu ziliimarishwa kwa wale wanaofundisha Dini au wanaolingania Uislamu, bila idhini ya serikali.
Wakati wa Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev alikutana na Rais wa Marekani Donald Trump, na makubaliano yalitiwa saini kati ya Marekani na Uzbekistan yenye thamani ya dolari bilioni 105 katika biashara ya pande mbili, kukuza uwekezaji, na unyonyaji wa rasilimali za madini za nchi hiyo. Hii iliiweka Marekani mbele ya China na Urusi katika ushirikiano wa kiuchumi na Uzbekistan.
Baada ya Taliban kutwaa madaraka nchini Afghanistan, sehemu kubwa ya ndege za kijeshi za Marekani, helikopta, na vifaa vya kijeshi vilihamishiwa Uzbekistan. Hivi sasa, serikali ya Taliban imeitaka Uzbekistan irudishe vifaa hivi vya kijeshi. Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump anaitaka serikali ya Taliban ikabidhi kambi ya kijeshi ya Bagram nchini Afghanistan kwa Marekani, lakini Taliban imekataa katakata. Haiwezekani kwamba Marekani itaacha vifaa vyake vya kijeshi nchini Uzbekistan na kubadilisha eneo hilo kuwa kambi ya kijeshi ya Marekani.
Asia ya Kati, hasa kitovu chake, Uzbekistan, imekuwa uwanja wa matarajio ya dola kubwa kama vile Urusi, China, Marekani, na Muungano wa Ulaya. Inaweza kugeuka wakati wowote kuwa bomu ambalo linaweza kulipuliwa na upande wowote, au pande zote kwa pamoja.
Enyi Waislamu:
Hakika, watawala wenu hawafikirii kuhusu ustawi wenu wa kiuchumi, kwani mko katika shida kubwa ya kiuchumi, na dola kubwa zinataka mjitenge na Dini yenu na kuwa wanafiki, wapagani, na makafiri kama wanavyotaka.
Kwa hivyo endeleeni kusimama imara katika Dini yenu, na msiwaruhusu watawala wenu kufikia nia hizi ovu. Jitahidini na fanyeni juhudi zenu zote ili kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, ambayo itakuongozeni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kwenye furaha ya dunia hii na Akhera na radhi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt),
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُون]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfaal: 24].
Na akaonya kwa kauli Yake (swt),
[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى * قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى وَقَدْ كُنتُ بَصِيراً * قَالَ كَذَلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا وَكَذَلِكَ الْيَوْمَ تُنسَى * وَكَذَلِكَ نَجْزِي مَنْ أَسْرَفَ وَلَمْ يُؤْمِن بِآيَاتِ رَبِّهِ وَلَعَذَابُ الآخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبْقَى]
“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa. Na hivi ndivyo tutakavyo mlipa kila apitaye kiasi, na asiye amini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi, na inadumu zaidi.” [Surah Taha 124-127].



