- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ummah Kati ya Uwepo Tu na Kazi Halisi, Kutokuwepo au Kutoweka? Sababu na Mbinu za Uchangamshaji
Na: Dkt. Ashraf Youssef Abu Ataya
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Al-Rayah - Toleo 570 - 22/10/2025
Kuna maswali yanayoulizwa kutoka kwa matukio ambayo Ummah unapitia mara kwa mara. Maswali hayo yanaongezeka kwa wakati huu, ambayo yanafanana na tuhma na kulaani kwa Ummah, kutokana na kuzingirwa na mauaji ya halaiki ambayo Gaza inateseka nayo, mikononi mwa Mayahudi wahalifu.
Ufahamu wenye nidhamu unaweza kujengwa tu juu ya msingi wa mitazamo iliyo wazi na fahamu maalum, zenye nidhamu, kwani kuhukumu kitu kunatokana na mtazamo wake. Ikiwa mitazamo ya pamoja haipo, ufahamu husambaratika na mawasiliano huwa magumu, ambapo huathiri uwezo wa kutambua uhalisia na kuchukua misimamo ya kivitendo kuhusiana na vitu, matukio, na watu. Kwa hivyo, fahamu za ukombozi na udhibiti zinawakilisha hatua ya msingi kwa ufahamu au mradi wowote wa mwamko.
Ni muhimu kutofautisha kati ya uwepo wa awali wa jambo na maelezo ya hali yake. Kwa mfano, uwepo wa kimwili wa gari ni wa kudumu, lakini kuharibika au kutotembea kwake kunaelezea hali yake. Vile vile, uwepo wa Ummah wa Kiislamu ni wa kweli na imara, wenye kumiliki vipengee vyake muhimu: Aqidah (itikadi) inayounganisha na mifumo ya maisha inayotokana na aqidah hiyo. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ]
“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Surah Al-Anbiyya: 92].
Kuuelezea Ummah kama dhaifu, uliosambaratika, isiokuwepo, au mgonjwa ni maelezo ya hali ya dharura ambayo haibatilishi uwepo kwake. Tofauti hii ni muhimu kwa sababu inatuondoa kutoka kwa dhana kwamba Ummah umepoteza misingi yake hadi kutambua kwamba upo lakini haufanyi kazi.
Kwa mtazamo huu, inaweza kusemwa kwamba Ummah wa Kiislamu leo upo lakini unakabiliwa na ulemavu wa utendaji. Wengi wako katika hali ya ukosefu wa ufahamu kifikra na kisiasa, huku harakati za mtu binafsi na athari zilizotawanyika zikijitokeza. Ummah umeteseka kutokana na udhaifu wa kifikra kutokana na ufahamu mdogo wa Uislamu kama kichocheo cha utambuzi, na kuuacha kuwa mawindo ya fahamu zilizoingizwa kutoka nje, na udanganyifu wa kifikra na kisiasa. Udhaifu huu na kujisalimisha kumesababisha kukosekana kwa vichocheo thabiti vya kifikra na kisiasa.
Kwa sehemu kubwa, makundi na vipote ima hayapo au yameoanishwa ndani ya uhalisia uliopo. Hili linafafanua ukosefu wa mwitiko wa pamoja kutoka kwa Ummah kwa matukio makubwa, kama vile mauaji ya halaiki na uhamishwaji mjini Gaza, ambapo pengo kati ya Ummah kama umbo lenye lengo na ufahamu wake wa kisiasa na ufanisi wake linaonekana kubwa.
Umbile la mgogoro wa Ummah haliko katika uwepo wake, bali katika ukosefu wake wa ufanisi wake. Kiini cha tatizo kiko katika kutokuwepo kwa fahamu kuu tatu:
- Kutokuwepo kwa fahamu za kuhamasisha: Aqidah (itikadi) ya Kiislamu sio tena msingi fikra na tabia.
- Kutokuwepo kwa nguvu zinazosukuma: Vyama vyenye ushawishi na vikundi vya kifikra na kitamaduni ima havipo au vimewekewa vikwazo.
- Kutokuwepo kwa uongozi wa kisiasa wa kimfumo, unaounganisha Ummah na kuelekeza nguvu zake.
Haya ndiyo yanayoashiriwa na kauli ya Mtume (saw) aliyesema, «إِذَا تَبَايَعْتُمْ بِالْعِينَةِ وَأَخَذْتُمْ أَذْنَابَ الْبَقَرِ وَرَضِيتُمْ بِالزَّرْعِ وَتَرَكْتُمْ الْجِهَادَ سَلَّطَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ ذُلًّا لَا يَنْزِعُهُ حَتَّى تَرْجِعُوا إِلَى دِينِكُمْ» “Pindi mnapofanya miamala ya ‘inah, na mukakamata mikia ya ng’ombe, na mukaridhia kilimo na kuachana Jihad, Mwenyezi Mungu atakusalitini na udhalilifu juu yenu ambao hatauondoa hadi mutakaporudi kwenye Dini yenu.”
Udhalilifu si kutokuwepo. Badala yake ni kusimama kwa dori ya kiutendaji na ufanisi, kutokana na kuitelekeza njia ya Kiislamu.
Njia ya uponyaji huanza kwanza kwa kufufua fahamu sahihi za Kiislamu katika utambuzi wa Ummah, kupitia kazi ya utetezi wa kifikra ambayo inaregesha ‘aqidah kwenye dori yake kama kichocheo kikuu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[قَدْ جَاءكُم مِّنَ اللّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ * يَهْدِي بِهِ اللّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلاَمِ]
“Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama.” [Surah Al-Maida:15]. Kazi hii kisha iendelea katika mfumo wa ushiriki wa kisiasa wa kimfumo ndani ya Ummah ili kuzalisha ufahamu jumla wenye nidhamu kuhusu Uislamu, kubadilisha hisia za watu kuwa rai jumla ya Umma ya kisiasa na kifikra, yenye uwezo wa kusukuma na kuelekeza matukio.
Pia lazima tuzungumzie udanganyifu wa vyombo vya habari na wa kisiasa unaozalisha ufahamu wa batili, na kufichua mbinu za kutengwa zinazoufanya Ummah kutotambua dori yake. Hapa, wajibu wa Sharia wa wale wanaobeba Dawah kwa Uislamu unaangaziwa. Ni uvumilivu, sio kuchoka au kuchoshwa, na kuendelea mchakato wa Dawah, kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu (swt) Ambaye amesema,
[وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّهِ]
“Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa sababu ya MwenyeziMungu tu.” [Surah An-Nahl:127].
Kuhamasisha vikosi vya jeshi bado ni kipengee muhimu katika kuregesha Ummah katika ufanisi, dori, na uongozi wake. Kazi yao ya Shariah si kulinda serikali zilizopo, bali badala yake ni kulinda Ummah na mradi wake mpana wa kisiasa, Khilafah. Mtume (saw) amesema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami.”
Kwa mtazamo wa Kiislamu, jeshi ni sehemu ya Ummah, na dhamira yake ni kuunga mkono mradi wake wa kisiasa, unaowakilishwa na Khilafah, ambayo huunganisha Ummah na kuregesha tamkini na ufanisi wake.
Kwa hivyo, Ummah wa Kiislamu upo wala haujamalizika. Badala yake, ni umbo lililopo kwenye misingi yake, lakini linakabiliwa na ulemavu wa utendaji. Ulemavu huu unatokana na kutokuwepo kwa fahamu, nguvu zinazosukuma, na uongozi wa kimfumo.
Kwa kuongeza juhudi za kampeni ya Dawah za kufufua fahamu za Kiislamu, kuunganisha utambuzi wa wahyi, kujenga rai jumla ya umma juu ya fikra ya kisiasa inayoongozwa na aqidah, na kuhamasisha nguvu fiche za Ummah, hasa majeshi, Ummah unaweza kuregesha uhai wake na dori yake ya kihistoria, kuregesha maisha yake ya Kiislamu, kurekebisha historia, na kurudi katika jinsi Mwenyezi Mungu (swt) alivyokusudia,
[وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُواْ شُهَدَاء عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا]
“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.” [Surah Al-Baqarah:143].



