Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 562
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ni masikitiko kwa usaliti! Maumivu yake yanaumiza moyo. Hakika, usaliti ni mchungu zaidi kwa nafsi kuliko maumivu ya njaa, kifungo, na mateso. Wananchi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina wakiwemo watu wa Gaza wanautaka Umma wa Kiislamu kuwanusuru na kuwakomboa, kwa sababu udugu wa Kiislamu unawataka Waislamu kuwanusuru wanaodhulumiwa miongoni mwao.
Tangu Disemba 8, 2024, Syria imeshuhudia ziara mbalimbali za kidiplomasia katika ngazi mbalimbali. Ziara hizi haziwezi kuelezewa kuwa ziara za kawaida, haswa baada ya kuchunguza historia ya nchi zilizo zuru Damascus na kuelewa uhalisia wake.
Vita vinavyoendelea katika sehemu mbalimbali za dunia—hasa vita kati ya Urusi na Ukraine na mzozo kati ya Iran na umbile la Kiyahudi—vinaonyesha wazi kwamba ulimwengu umeingia katika awamu mpya na tofauti ya vita vya kijeshi na kijasusi. Mtazamo wa kale wa vita, uliopitwa na wakati, unaojengwa juu ya vikosi vikubwa vya askari wachanga, vifaru, na mizinga, unabadilika kwa kasi na kuporomoka. Leo, dola kama vile Marekani, China na Urusi zinatenga bajeti kubwa kwa viwanda vya juu vya kijeshi na zinafafanua upya mbinu mpya za kivita. Vita kwenye mstari wa mbele wa kisasa havikomei tena kwa risasi na bunduki – ni vita vya operesheni za kimahesabu (algorithms), akili ya bandia, droni, mtandao na mawimbi ya satelaiti.