Ijumaa, 16 Muharram 1447 | 2025/07/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Indonesia: Katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa kwa Khilafah “Palestina itakombolewa kupitia Khilafah na Jihad”

Kwa mnasaba wa kumbukumbu (miaka 104 H) ya kuvunjwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu 1342 H sawia na 03/03/1924 M mikononi mwa wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, na kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) yaliyofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina), Hizb ut Tahrir / Indonesia iliandaa matembezi makubwa katika mji mkuu wa Jakarta yenye kichwa “Palestina itakombolewa kupitia Khilafah na Jihad”.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Mabadiliko Mapya ya Kisiasa nchini Lebanon

Ni yapi yanayojiri nchini Lebanon kuhusu wepesi wa makubaliano juu ya uteuzi wa Kamanda wa Jeshi Joseph Aoun kama rais mnamo 9 Januari 2025 baada ya nafasi hiyo kudumu kuwepo kwa zaidi ya miaka miwili, kisha siku chache baadaye makubaliano kwa Salam Nawaf kuwa kama waziri mkuu mnamo 13 Januari 2025? Haya yote yalitokeaje haraka hivyo? Je, kasi hii ina maana kwamba kazi ilikuwa na bado ingali inatayarishwa kubadilisha uso wa Lebanon ndani na nje, au ni mabadiliko ya kawaida, kama inavyotokea katika kanda hiyo?

Soma zaidi...

Hatari ya Uhamisho Inayotafutwa na Trump na Umbile la Kiyahudi Inalazimu Hatua Kali katika Kuamiliana nao kama Maadui

Utawala wa Jordan na kundi la watu wake wakati wote wa vita vya Kiyahudi dhidi ya Gaza walikuwa na bado wangali wanatetea kutowanusuru watu wa Gaza kijeshi, na angalau sio kufutilia mbali makubaliano ya udhalilishaji na aibu na umbile la Kiyahudi, lakini kwa busara na hekima na ujanja wa kisiasa hii ni hatua na udhoofishaji wa amani, usalama na chemchemi ya utulivu ambayo Jordan inaishi ndani yake. Mfalme alifikiri kwamba Uingereza ilimuamuru kurukuu na kujibu ajenda ya Amerika ambayo imelitawala eneo hilo tangu aingie madarakani, kufuatia mbinu ya baba yake, na kile ilichomuagiza kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya ulinzi nayo mwaka 2021 ambayo yanahujumu kila maana ya ubwana wa nchi yoyote, na kuifungua nchi kwa ujumla kwa kambi za Amerika pekee na viwanda na vikosi vyake.

Soma zaidi...

Kuganda Baridini hadi Kufa kwa Watoto Wachanga, na Njaa na Uuaji wa Watoto Hayatoshi Kukomesha Mauaji ya Halaiki huko Gaza!

Mnamo tarehe 30 Disemba, iliripotiwa kuwa mtoto wa 6 waliganda hadi kufa mjini Gaza ndani ya wiki mbili kutokana na hali ya baridi inayovumiliwa na wakimbizi wa Kipalestina katika mahema ya muda, waliohamishwa kutoka kwa nyumba zao kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Ukanda huo na uvamizi wa Kiyahudi. Ali al-Batran mwenye umri wa mwezi mmoja alifariki siku moja baada ya kaka yake pacha, Jumaa al-Batran, huko Deir el-Balah. Baba yao, Yahya Muhammad al-Batran, alisema kuwa Jumaa alipatikana kichwa chake kikiwa kama “donge la barafu”. Nariman, mama wa Sila Mahmoud al-Fassih mwenye umri wa siku 20, ambaye pia alifariki kutokana na kupungua kwa joto la mwili, alielezea kumkuta mtoto wake akiwa rangi ya bluu na kuuma ulimi wake huku damu ikimtoka mdomoni. Zaidi ya watu milioni 1.6 wa Gaza wamelazimishwa kuingia kwenye makaazi ya muda, wakiishi katika mahema hafifu ambayo hayatoi ulinzi kutokana na hali ya hewa ya baridi kali.

Soma zaidi...

Wauyghur Pia Ni Sehemu ya Umma Bora, Musiwasahau

Tunapokaribia kumbukumbu ya mwaka wa 104 wa kuvunjwa kwa Khilafah, Umma wa Kiislamu unaendelea kupokea habari za ukandamizaji kutoka kwa maadui wake kila mahali, kuanzia Palestina hadi Syria, Sudan, Misri na China, ambako Waislamu wa Uyghur wanavumilia mateso na vikwazo vikali katika kila nyanja ya maisha yao.

Soma zaidi...

Machafuko na Ghasia nchini Sudan Kusini Zinasisitiza Haja ya Umma kuwa na Kiongozi mwenye Kuwalinda

Ulimwengu umefuatilia machafuko ya Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ambayo yalilenga watu waliokimbia makaazi yao na wakaazi kutoka Sudan Kaskazini. Matukio haya yalichochewa na ripoti zinazowatuhumu wanajeshi wa Sudan kwa kuwaua watu kutoka Sudan Kusini huko Wad Madani baada ya jeshi kuutwaa tena mji huo. Kulingana na gazeti la ‘Sudan Tribune’, Wasudan watatu waliuawa mjini Juba, na wengine saba kujeruhiwa.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu