Jumanne, 24 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  22 Rabi' I 1447 Na: H 1447 / 11
M.  Jumapili, 14 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh Yawaalika Watu Wote Watambuzi, wakiwemo Wanasiasa, Wasomi, Waandishi wa Habari na Kizazi cha Vijana cha Nchi Kutazama Kongamano lake la Kisiasa Mtandaoni lenye Kichwa “Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?”

(Imetafsiriwa)

Licha ya kuanguka kwa dhalimu Hasina kwa gharama ya mihanga mingi ya watu, matumaini na matarajio ya watu hayajatimia. Mnashuhudia kwamba Marekani-Uingereza-India wanaingilia waziwazi katika siasa za Bangladesh na kula njama za kukwamisha matarajio ya wananchi katika uasi huo. Serikali ya mpito, mlinzi wa kirongo wa uasi huo, inawahadaa watu kwa jina la ‘mageuzi ya serikali’, ‘mageuzi ya katiba’, ‘Azimio la Julai’, ‘Mkataba wa Julai’ na inajishughulisha na kutekeleza ajenda ya Marekani. Badala ya kutimiza matarajio ya wananchi kwa ‘Bangladesh Mpya’ (Bangladesh: 2.0), kwa sasa wana shauku ya kudumisha mwendelezo wa utawala wa Hasina. Katika muktadha huu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, imeandaa kongamano la kisiasa la mtandaoni lenye kichwa “Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?” kutoa mwongozo kwa wananchi ili kufikia lengo kuu la Mapinduzi ya Julai 24. Munaalikwa kutazama kongamano hili ili kupata mwamko wa kisiasa na kuamua nini cha kufanya katika hatua hii ya kisiasa nchini. Maelezo ya kongamano hilo ni kama ifuatavyo:

Tarehe na Wakati:

19 Septemba 2025

Ijumaa, 7 PM

Tovuti ya Matangazo:

ALWAQIYAH.TV

Hotuba katika kongamano:

Hotuba 1: Marekani-Uingereza-India Zala njama kukwamisha Majarajio ya Watu katika Uasi wa Julai

Hotuba ya 2: Bangladesh 2.0: Njia ya Kutokana na Dhulma ya Ukoloni Mamboleo na Mfumo wa Kisekula wa Kibepari

Hotuba 3: Mwongozo kwa Watu kusaidia Uasi kufikia Lengo lake Kuu

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Bangladesh

 

Bonyeza Hapa Kufuatilia Ukurasa wa Kongamano

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu