Jumanne, 24 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  23 Rabi' I 1447 Na: H 1447 / 12
M.  Jumatatu, 15 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sehemu za dhati za nchi Lazima Ziungane dhidi ya Sera ya Serikali ya Mpito ya Utiifu kwa Marekani Mkoloni Kafiri

(Imetafsiriwa)

Serikali ya mpito inaisaliti nchi kwa kuonyesha kusitasita kulinda Mipaka yetu kutoka kwa ‘Jeshi la Arakan’ linaloungwa mkono na Marekani, huku ikitamani kuwatumia wanajeshi wetu kwa Misheni ya Amerika nchini Ukraine. Kuanzia Disemba 2024 hadi Septemba 10, kundi la waasi lenye makao yake nchini Myanmar liliwateka nyara wavuvi 325 kutoka maeneo mengi kando ya Mto Naf na Ghuba ya Bengal. (bdnews24.com, Septemba 12, 2025). Kinaya ni kwamba, serikali ya Yunus ilipuuza Jeshi la Arakan (wakala wa Marekani) linalofanya kazi ndani ya ardhi yetu na kutishia watu wetu na ubwana wetu. Wakati huo huo, ilikuwa haraka kuisaidia Ukraine ili kumfurahisha bwana wake wa ubeberu mamboleo, Marekani. Marekani inafikiria kupeleka askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo salama (buffer) kati ya Urusi na Ukraine iwapo makubaliano ya amani yatakamilika. Wanajeshi kutoka nchi zisizo za NATO, kama vile Bangladesh, wanaweza pia kutumwa, NBC News inaripoti. Mshauri wa Mambo ya Nje wa serikali ya mpito ya Bangladesh, Touhid Hossain, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Bangladesh ingependa kushiriki katika operesheni yoyote kama hiyo. Kando na hilo, Kikosi cha Usalama cha Mipaka ya India (BSF) pia kinaendelea kuua watu wetu katika maeneo ya mpakani, na watu zaidi wameuawa katika miezi ya hivi karibuni, wakati serikali yetu wenyewe haifanyi chochote kuwalinda. Kwa hivyo, ni unafiki wa hali ya juu kwamba serikali yetu inataka kuajiri askari tunaowahitaji nyumbani kucheza kijana wa kazi kwa ajili ya Magharibi.

Enyi Maafisa Wanyoofu wa Jeshi la Bangladesh, tunasisitiza na tunaendelea kuwakumbusha kwamba misheni hizi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa si chochote ila zana za ukoloni mamboleo unaoongozwa na Marekani. Hizi hutumika kuvuruga maeneo na kupata rasilimali na mali za kimkakati kwa ajili ya mfumo wa ulimwengu wa Magharibi unaoongozwa na Marekani. Kwa kushiriki katika miradi hii, munakuwa washiriki katika miradi ya kibeberu ya wapiganaji makafiri. Enyi maafisa, watawala wetu wadanganyifu wamekufanyeni mchezo usio na maana wa mfumo wa ulimwengu wa kibepari wa Magharibi. Kwa ulafi wa kupata fedha kidogo za kigeni na kwa matumaini ya uaminifu wa Magharibi, wanataka kukusahaulisheni zama zenu za Izza. Ni jeshi la Kiislamu pekee hapa duniani ambalo limewakomboa wanadamu kutoka katika giza la makafiri tangu zama za Mtume Muhammad (saw). Jeshi la Khilafah Rashida halikujifungia ndani ya mipaka yake yenyewe, bali pia liliuweka nusu ya ulimwengu chini ya kivuli cha Uislamu kupitia jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Hata hivyo, leo watawala hawa wamekufikisheni kwenye hali duni sana kiasi kwamba munashindwa hata kulinda mipaka yenu wenyewe, achilia mbali dunia nzima. Jeshi la Khilafah kamwe halikuwahi kutafuta maisha ya anasa kama vile askari mamluki wa dola za Kirumi na Fursi kwa malipo ya dhahabu na fedha. Lakini la kusikitisha, watawala wetu wadanganyifu wamekufanyeni mupate madolari katika misheni ya UN kama sababu ya fahari yenu. Tazameni jinsi watawala wa dola za kitaifa wamekushusheni leo! Tunakuombeni muinusuru Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah Rashida iliyoahidiwa kwa njia ya Utume. Lengo lenu pekee maishani linapaswa liwe kucheza dori muhimu katika kuhuisha Khilafah na kuziondoa dola za kikafiri za Magharibi na mfumo wao wa dunia. Kumbukeni, hakuna kizazi chengine kilichowahi kupata fursa hii adhimu ya kuhuisha Uislamu kikamilifu katika kipindi cha miaka 1400 tangu zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia. [Sura As-Saff:9].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu