Doria ya Pamoja ya 'CORPAT' na Adui India na Zoezi la Pande Mbili 'Bangosagar' Inathibitisha kuwa Vibaraka wa Marekani-India Wanacheza na Ubwana wa Nchi kwa Maslahi ya Mabwana zao Wakoloni
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Moja ya sababu zilizomfanya msaliti Hasina kupinduliwa na watu ni kwamba alitekeleza njama ya India kule Pilkhana na mara kwa mara alifanya majaribio mabaya yote ya kuweka udhibiti wa India juu ya jeshi la nchi hiyo. Wakati ambapo wananchi wanapaza sauti kudai haki kwa mkasa wa Pilkhana, doria ya pamoja 'CORPAT' na zoezi la pande mbili 'Bangosagar' lililofanyika katika Ghuba ya Bengal kwa kushirikisha jeshi la wanamaji la Bangladesh na India imewashtua watu. Kwa kweli, vibaraka wa Marekani-India wamedhamiria kulinda maslahi ya kijiografia ya wakoloni wao hata kwa gharama ya ubwana wa nchi. Inafaa kutaja kwamba wakati matabaka ya kisiasa ya kisekula ya nchi hayakupaza sauti yake dhidi ya njama hiyo ya Pilkhana, ni Hizb ut Tahrir pekee ndiyo iliyofichua njama hiyo mbele ya taifa hilo kwa ushujaa na kupinga njama hiyo dhidi ya ubwana wa nchi hii.