Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 534
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ripoti ya jibu la swali lililotolewa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, kuhusu Kuongezeka kwa Uhasama nchini Sudan.
Ramadhan ni mwezi ambao ndani yake Umma wa Kiislamu ulishinda maadui wengi wenye nguvu. Hebu Waislamu na waregeshe hukmu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ﷻ katika mwezi wa Ramadhan, na warudishe ushindi dhidi ya maadui, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu ﷻ.
Hii ni video iliyoelekezwa kwa wanasiasa wa Sweden kuhusu tishio linaloongezeka kwa Waislamu baada ya maneno ya chuki. Inakuja kama jibu kwa ufyatuaji risasi wa hivi punde wa shule huko Örebro.
Al Arabiya Net ilichapisha kwenye tovuti yake mnamo tarehe 4/2/2025: "Jeshi na vikosi vyake vya usaidizi viliingia katika maeneo ya kusini-mashariki ya Jimbo la Khartoum wakati wa saa zilizopita, wakitokea Jimbo la Al-Jazeera.." na tovuti ya Youm7 ilichapishwa mnamo tarehe 2/2/2025: "Mwandishi wa Kituo cha Habari cha Cairo aliripoti katika habari mpya zinazochipuka kwamba jeshi la Sudan linachukua idadi kadhaa ya vijiji mashariki mwa mto Nile katika Jimbo la Khartoum." Kabla ya hapo, mnamo tarehe 11/ 1/2025, Vikosi vya Msaada wa Haraka vilishindwa na jeshi la Sudan katika mhimili wa Jimbo la Al-Jazeera na mji mkuu wake, Wad Madani, “na kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Hemeti, alikiri katika kanda ya sauti iliyohusishwa naye kwamba vikosi vyake vilishindwa katika Jimbo la Al-Jazeera...” (Al-Jazeera 1/13/2025).
Dola ya Kibaniani Yawaua Mujahidina katika Kashmir Inayokaliwa Kimabavu baada ya Dola ya Pakistan Kuwatelekeza!
Ripoti ya jibu la swali lililotolewa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, kuhusu Juu ya juhudi za kutaka watu wa Gaza wahame kutoka katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina).
Video hii pia inazungumzia jinsi ushindi na mafanikio ya kweli kwa nchi ya Syria na kwengineko yanaweza kupatikana tu kupitia kuziondolea ardhi zetu mabaki yote ya uingiliaji kati na utawala wa wakoloni - ikiwemo vipengele vyote vya mfumo wao wa kisiasa na imani, na kuikumbatia ruwaza ya kweli ya Kiislamu iliyo huru. Hili linaweza kupatikana tu kwa kutekeleza Sheria na Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ukamilifu chini ya kivuli cha Khilafah kwa njia ya Utume.
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 104 Hijria ya kuvunjwa dola ya Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu mwaka 1342 H sawa na 03/03/1924 M mikononi mwa wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, na kwa kuzingatia mabadiliko na mishtuko mikali inayotokea ndani na karibu na ardhi ya Ash-Sham, Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon inaandaa kongamano lenye kichwa: “Mabadiliko katika Ardhi ya Ash-Sham... Wasiwasi na Bishara!”