Jumatano, 22 Safar 1448 | 2026/08/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Amali na Shughuli katika Mwezi wa Juni 2026 M

Hizb ut Tahrir / Sudan iliimarisha shughuli zake za umma wakati wa mwezi wa Juni 2026, ikiuhimiza Ummah kufanya kazi nayo ili kuanzisha jengo kubwa la Uislamu: Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Shughuli maarufu zaidi za Hizb ut Tahrir katika wilayah ya Sudan zilikuwa kama ifuatavyo:

1/ Mizizi ya Usekula katika Siasa za Sudan na Jinsi ya Kuiondoa

Baada ya kutokuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na vita, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan ilifanya shughuli zake za kwanza za kisiasa katika afisi yake katikati mwa jiji la Khartoum mnamo Juni 6, 2026. Iliandaa Jukwaa lake la Masuala ya Ummah la kila mwezi, lililohudhuriwa na idadi kubwa ya waandishi wa habari, wanasiasa, na wale wanaopenda masuala ya umma. Jukwaa hilo lilizungumzia mizizi ya usekula katika siasa za Sudan na jinsi ya kuiondoa.

Dkt. Ahmed Abdel-Fadil alizungumza katika jukwaa hilo, akielezea mizizi ya usekula nchini Sudan, akielezea kwamba iliingia na wakoloni wa Uingereza na imeendelea kuwa kubwa hadi leo. Kuhusu kwa nini inajadiliwa kwa kina siku hizi katika duara za kisiasa na hata kijeshi, ni kuihalalisha na kugeuza mjadala wowote kuhusu Uislamu na hukmu zake kuhusu utawala na siasa. Alihitimisha kwa kusema kwamba usekula ni mfumo wa kikafiri, na utekelezaji na ulinganiaji wake ni haramu.

Kisha, Ustadh Abdullah Hussein, mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, aliwasilisha masuluhisho yanayozingatia Sharia za kutokomeza usekula. Maingiliano yalikuwa mazuri, huku idadi ya waliohudhuria wakishiriki, wakitoa maoni, na kusisitiza umuhimu wa kufanya kazi kuelekea Khilafah.

 2/ Kushindwa kwa Dola Kulinda Miji ya Sudan

Mnamo Juni 14, 2026, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mashambulizi dhidi ya matembezi ambayo mji wa El Obeid umefanyiwa mara kwa mara, huku dola ikipuuza kuulinda. Baadhi ya sauti katika vyombo vya habari zimeibuka zikiwataka watu wa Kordofan kujilinda. Msemaji rasmi alifafanua katika taarifa yake kwamba kudumisha usalama na kutoa maisha yenye hadhi ni miongoni mwa majukumu ya dola, kwani ni dola inayosimamia mambo na kutoa usalama, ikiichukulia kama wajibu wa kidini, sio fadhila kutoka kwa dola. Anayeizuia dola kutekeleza wajibu wake ni yule anayepanga vita hivi vya kipuuzi na vilivyolaaniwa, yule anayetaka kutenganisha Darfur na mwili wa Sudan. Hii ni Amerika, ambayo inajitahidi kuigawanya Sudan kwa kuwachosha watu wake.

3/ Kuendelea kuporomoka kwa pauni ya Sudan kunathibitisha kufeli kwa serikali kushughulikia mgogoro huo.

Katikati ya kushuka kwa kasi kwa thamani ya sarafu ya ndani dhidi ya sarafu zengine, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan alitoa taarifa akifichua sababu za kushuka huku kwa kutisha. Miongoni mwa sababu hizi ni kigingi cha sarafu ya ndani kwa dolari. Alisema kwamba Khilafah itaegemeza sarafu yake kwa dhahabu, si dolari, na hivyo kuipa thamani ya dhati ambayo inaweza kutumika katika biashara ya kimataifa, uagizaji na usafirishaji. Aliongeza kuwa mapato ya dhahabu, kama mali ya umma, yatatengwa kwa huduma za maji, umeme, miundombinu, na huduma zengine muhimu. Alisema kwamba sisi katika Hizb ut Tahrir/Wialayah ya Sudan tunathibitisha kwamba Sudan, pamoja na rasilimali zake nyingi, ni tajiri na watu wake hawawezi kufa njaa. Hata hivyo, inahitaji mfumo unaosimamia rasilimali hizi kwa manufaa ya watu, si kwa manufaa ya adui, watawala, na marafiki zao. Mfumo huu upo tu katika Uislamu, chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

4/ Suluhisho Msingi kwa Mgogoro wa Kiuchumi

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan ilimkaribisha Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika afisini kwake katika mji mkuu wa utawala, Port Sudan. Mkutano huo, uliopewa jina la "Suluhisho Msingi kwa Mgogoro wa Kiuchumi," ulishughulikia sababu kuu za matatizo yanayoukumba uchumi wa Sudan. Hizi ni pamoja na ukweli kwamba mfumo wa kiuchumi wa Sudan umejengwa juu ya ubepari, ambao hauna mbinu inayotegemea ustawi, na kwamba mfumo huu unatekelezwa katika hali yake mbaya zaidi, huku dola za kikoloni zikidhibiti sera za kiuchumi kupitia Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia. Sababu zengine zinazochangia ni kuelea kwa sarafu ya ndani, na kusababisha kushuka kwake. Alisema kwamba mambo haya, yakichukuliwa pamoja, yanasababisha kubomolewa kwa serikali ili kutumikia maslahi ya makafiri, wakoloni wa Magharibi.

Kisha akaeleza kwamba suluhisho msingi la mgogoro wa kiuchumi nchini Sudan, na kwa hakika duniani, liko katika hukmu za Uislamu kama zinavyotekelezwa na Khilafah, ambayo hutoa maisha yenye heshima kwa watu wake. Alitoa wito wa kufanya kazi kwa bidii bidii pamoja na wanachama waaminifu wa Ummah ili kurudisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

5/ Hotuba za Kisiasa jijini Port Sudan

Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan imekuwa ikitoa hotuba ya kisiasa ya kila wiki kila Jumatatu katika mji mkuu wa utawala, Port Sudan. Hotuba za mwezi huu zilikuwa chini ya vichwa vifuatavyo:

A/ Matumizi ya Ukabila Kugawanya Sudan

Katika hotuba hii, Ustadh Adel Ibrahim alizungumza, akielezea uharamu wa ukabila na kujisifu kuhusu hilo, na kwamba dhamana iliyoanzishwa na Uislamu ni dhamana ya udugu wa Kiislamu, ambayo huunganisha makabila mbalimbali na kuwafanya kuwa ndugu. Kisha akaeleza kwamba ukabila katika Uislamu hutumika kuhifadhi nasaba, kudumisha uhusiano wa kidugu, na kuhakikisha mwendelezo wa miunganisho ya kifamilia. Alisema kwamba kusudi la awali la makabila lilikuwa kuinuka na kushindana katika kunusuru Uislamu, kama vile makabila ya Aws na Khazraj yalivyoimarisha dini, kumnusuru Mtume, na kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu. Alieleza zaidi kwamba ukabila unatumiwa vibaya na mkoloni kafiri ili kupanda mbegu ya mgawanyiko miongoni mwa Waislamu na kugawanya ardhi zao, na kusababisha kujitenga kwa Sudan Kusini. Sasa, hisia zile zile za kikabila na kikanda zinatumika kutenganisha Darfur.

B/ Hijra ya Mtume Inamaanisha Kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu:

Ustadh Hussein Al-Hadi alizungumzia mada hii, akianza na mipango iliyokamilishwa Medina katika maandalizi ya kuanzisha dola ya Kiislamu. Mipango hii ilimpa Mtume (saw), na uhamiaji huo ulikusudiwa kuanzisha mamlaka ya Uislamu. Mamlaka haya yakawa ya kujitawala, na sheria ya Kiislamu ikatekelezwa, na hivyo kuifanya Medina kuwa makao ya Uislamu na Waislamu. Alitoa dalili ya hili. Kisha akaelezea jinsi makafiri walivyoharibu mamlaka haya baada ya karibu karne kumi na nne ambapo Waislamu walikuwa na dola na Khilafah. Alimalizia kwa kusisitiza umuhimu wa kuanzisha tena mamlaka haya ili Waislamu waweze kutekeleza hukmu za Uislamu na kuipeleka dini hii duniani, hivyo kutimiza kusudi ambalo umma wa Kiislamu ulichaguliwa kama umma bora zaidi ulioletwa kwa ajili ya watu.

C/ Ubwana wa Sheria ya Kiislamu

Chini ya kichwa hiki, hotuba ya kila wiki ilifanyika katika soko kubwa la Port Sudan. Ustadh Yaqoub Ibrahim alizungumza, akielezea umuhimu wa ubwana wa sheria ya Kiislamu katika mambo ya umma, dola, na watu binafsi. Alisema kwamba hii ndiyo kanuni ya kwanza ya utawala katika Khilafah ya Kiislamu. Alitoa mifano ya mahusiano yanayofanywa nje ya Uislamu katika maisha ya watu, iwe ni mahusiano yao na dola au wao kwa wao, na jinsi watu wameshindwa kutambua kwamba ubwana ni wa sheria ya Kiislamu. Kisha akawawajibisha watu kwa kusimamisha mfumo wa Khilafah, ambao ungehakikisha ukuu wa sheria ya Kiislamu, akiuchukulia kama wajibu wa lazima. Mchango mkubwa ulitoka kwa mkaazi wa mashariki mwa Sudan, ambaye alitoa maoni kuhusu umuhimu wa kutekeleza mfumo wa Kiislamu na ubwana wa sheria na dini ya Kiislamu, vyenginevyo, watu wanapaswa kutarajia hasara dhahiri Akhera.

D/ Masomo Yaliyopatikana kutoka kwa Ashura

Ustadh Adel Ibrahim alizungumza, akielezea ubwana wa siku hii, ambayo Mtume (saw) aliwahimiza Waislamu kufunga. Siku hii, Mwenyezi Mungu alimwangamiza Farauni na kumwokoa Nabii Wake Musa (amani iwe juu yake) na waumini pamoja naye. Alisema kwamba kila zama zina Farauni wake, na kwamba Farauni wa zama hizi ni Amerika, ambayo hueneza ufisadi duniani kupitia mauaji na uharibifu. Alidai kwamba Waislamu pekee ndio wanaweza kuzuia kiburi hiki, kwa hivyo lazima wachukue hatua zinazohitajika na kujitolea kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha dini na kisha kuipeleka ulimwenguni ili kuwatoa watu gizani na kuwaingiza nuruni. Hili linaweza kupatikana tu chini ya Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Wahudhuriaji, wakiwemo wenye maduka na wachuuzi, walisikiliza kwa makini, na maingiliano yao na hotuba yalikuwa mazuri.

6/ Mauaji Kwenye Mipaka ya Sykes-Picot

Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan alitoa taarifa akizibebesha ndani yake serikali za Misri na Sudan kuwajibika kwa matukio ya kusikitisha yaliyotokea kwenye mpaka wa Sudan na Misri. Taarifa hiyo ilitangaza kwamba damu ya waliokufa na kujeruhiwa wasio na hatia ilikuwa mikononi mwao, na kusisitiza kwamba unyanyasaji kama huo kwa wachimbaji madini wasio na hatia, hata kama wahalifu walikuwa miongoni mwao, ni kitendo ambacho hakijaidhinishwa na sheria ya Kiislamu. Hii ilikuja baada ya ndege za Misri kuwapiga mabomu wachimbaji madini ya dhahabu katika maeneo ya Jabal al-Ahmar na Jabal Ayqad. Jeshi la Misri lilikiri kitendo chake cha kinyama, huku msemaji wake akisema katika taarifa mnamo Juni 22, 2026: "Jeshi la Misri na vipengee vya Wizara ya Mambo ya Ndani vilifanya kampeni kubwa katika eneo la kusini dhidi ya maeneo yenye wahalifu wanaojihusisha na shughuli haramu, ikiwa ni pamoja na biashara haramu ya dawa za kulevya na silaha, uchimbaji haramu wa dhahabu, na uhamiaji haramu!"

Msemaji huyo alisema katika taarifa yake kwamba hamu ya serikali hizi vibaraka kudumisha mipaka iliyochorwa na mkoloni kafiri, na kuilinda kwa ndege na silaha nzito, ambazo zinaelekezwa kwenye vifua vya wana wa umma badala ya kwenye vifua vya maadui, inalazimisha umma kukataa serikali hizi na kusimamisha mfumo wa Uislamu; Khilafah, ambao unaondoa mipaka hii. Asili ni kwamba Sudan na Misri ni nchi moja, ambayo iligawanywa na mkoloni kafiri, Muingereza, ambaye aliunda serikali za kulinda mipaka hii.

 7/ Vita vya Kizazi cha Nne na Mmomonyoko wa Polepole wa Dola ya Sudan

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Sudan ilifanya jukwaa la kisiasa Jumamosi, Muharram 12, 1448 H (Juni 27, 2026 M). Jukwaa hilo lilimshirikisha Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir nchini Sudan, ambaye alijadili kwa undani vita vya kizazi cha nne, waratibu wake, malengo, na zana. Alielezea kwamba ni njama ya kuvunja dola kupitia mmomonyoko wa taratibu. Kisha akageukia dola ya Sudan, akielezea kwamba kinachoendelea ni sehemu ya mpango wa ugawanyaji. Aliwatambulisha wale wanaoipanga na kufichua zana zake za ndani, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kiraia, tawala za mitaa, harakati za kijeshi, viongozi wa kijeshi, na baadhi ya wanasiasa. Alisisitiza dori ya siri ya vyombo vya habari katika kupotosha maoni ya umma na kuunda mazingira yanayofaa kwa vita vya kizazi cha nne.

Alimalizia kwa kusema kwamba suluhisho liko katika kutekeleza Uislamu, ambao huondoa mambo haya yote kupitia hukmu za Sharia, kama vile kuzuia kuwa na majeshi mengi (ya nchi nyingi), kukataza ukabila, kuharamisha makundi ya kikabila na kikanda, kuzuia mashirika ya kikoloni kuingilia mambo ya nchi, na hukmu zengine zinazoweka utulivu. Alisema kwamba suluhisho msingi ni kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

8/ Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkutano wake wa kawaida katika jiji la Al-Qadharif siku ya Jumamosi, Muharram 5, 1448 H (Juni 20, 2026 M), ambapo ilijadili tatizo la maji mjini Al-Qadarif na kuwasilisha masuluhisho ya Kiislamu. Ustadh Al-Mahi Abdeen alizungumzia kufeli kuendelea kwa serikali zilizofuata, alijadili historia ya mgogoro wa maji wa Al-Qadarif, na ahadi zinazorudiwa ambazo zimezidisha tatizo na kuongeza mateso. Pia alizungumzia kuhusu mtandao wa zamani wa maji na kutoweza kwake kukidhi mahitaji ya watu kutokana na upungufu wake kwa idadi ya watu, pamoja na kukatika kwa laini. Kisha, Ustadh Abdul Majeed Mustafa alizungumzia masuluhisho ya Uislamu kupitia hukmu zake za kisheria, akielezea kwamba sheria ya Kiislamu pekee ndiyo inayoweza kushughulikia matatizo yote ya wanadamu. Alisisitiza kwamba maji ni uhai na moja ya mahitaji msingi ambayo kila mwanadamu anapaswa kupata. Alisema kwamba ni rasilimali ya umma, na kwamba mtawala analazimika kuyatoa kwa kila mtu miongoni mwa raia wake. Aliona kutoa maji ya kunywa kuwa moja ya majukumu muhimu zaidi ya serikali, na kwamba kuakhirisha mambo na kuchelewesha mambo kama hayo ni upuuzi mkubwa zaidi ambao serikali inaweza kufanya dhidi ya raia wake. Alibainisha kuwa dola vibaraka zilizoanzishwa na Makafiri wa Magharibi katika ardhi zetu zinaweka kuwahudumia watu chini ya vipaumbele vyao, zikichukua hatua tu wakati mapungufu yao yanapofichuliwa. Kisha huwatuliza watu kwa masuluhisho ya viraka, zikiwavuruga huku wakijitolea kumtumikia mkoloni kafiri na kulinda maslahi yake. Alitoa wito wa kufanya kazi kuelekea kuanzishwa kwa Khilafah, ambao ungesimamia mambo kulingana na hukmu za Uislamu.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan

Jumanne, 15 Muharram Tukufu 1448 H sawia na 30 Juni 2026 M

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu